Tiba za Jadi za Kabila la Wamiao
中国国际广播电台

    Tiba za jadi za kabila la wamiao zinaona kuwa sumu, udhaifu, jeraha, chakula kulundikana tumboni, vijidudu na wadudu ni aina 6 za vitu vinavyoathiri afya ya watu na kuwafanya kuugua ugonjwa.

Nyingi za dawa za jadi za kabila la wamiao zinatengenezwa kutokana na mimea, wanyama na aina chache za madini. Kutokana na takwimu zisizokamilika, hivi sasa dawa za jadi za kabila la wamiao zimefikia aina zaidi ya 1,500, aina 200 kati ya hizo zinatotumika mara kwa mara.

Dawa za jadi za kabila la wamiao zinapatikana kwenye milima ya Miaoling, Wumeng na Wuling. Katika miaka ya karibuni kwenye maeneo wanayoishi watu wa kabila la wamiao vimeanzishwa vituo vya uzalishaji wa dawa za jadi.