Enzi ya Xia
中国国际广播电台

Enzi ya Xia ni enzi ya kwanza katika historia ya China, ambayo ilikuweko kwa miaka karibu 500 kati ya karne ya 21 kabla ya Kristu na karne ya 16 kabla ya Kristu.

Enzi ya Xia ilianzishwa na shujaa Da Yu ambaye alitengeneza miradi ya maji ya kunufaisha watu. Inasemekana kuwa alifungwa mkono na watu wa eneo lake kutokana na kufanikiwa kurekebisha mtu Manjano uliofurika na kuleta maafa mara kwa mara, na hatimaye alianzisha enzi ya Xia, tokea hapo China iliingia jamii yenye utaratibu wa kitumwa.

Mwishoni mwa enzi ya Xia, ufisadi wa kisiasa ulikithiri katika utawala wa mfalme, hususan mfalme wa mwisho Xia Jie alijua kuponda raha tu wala hakujali hali ya shida ya watu. Mwishoni jeshi lake lillishindwa na waasi, na enzi ya Xia ikaanguka.

Wataalamu wa historia wana maoni tofauti kuhusu kuweko enzi ya Xia kutokana na data kidogo zisizokamilika. Tokea mwaka 1959 wataalamu wa mabaki ya kale walianza kufanya uchunguzi kuhusu “magofu ya enzi ya Xia”. Hivi sasa wataalamu wengi wanaona kuwa magofu ya Erlitou mkoani Henan ni vitu muhimu kwa utafiti kuhusu utamaduni wa enzi ya Xia.

Vyombo muhimu vya kazi za uzalishaji vilivyofukuliwa katika magofu ya Erlitou ni vyombo vya mawe ingawa vyombo vya aina nyingine vya pembe na mifupa ya mwanyama pamoja na kauri za baharini pia zilitumika. Ingawa watu hadi hivi leo bado hawajaona vyombo vikubwa vya shaba nyeusi vilivyofukuliwa kutoka kwenye magofu ya enzi ya Xia, lakini kulikuwa na vyombo na silaha za shaba nyeusi zikiwemo visu, patasi, tindo, vichwa vya mishale na vyombo vya kunywea pombe.

Katika kumbukumbu zilizoandikwa vitabuni, kitu muhimu ni matumizi ya kalenda katika enzi ya Xia. Hii inaonesha kuwa wakati ule watu waliweza kujua miezi kutokana na mahali zilipofika na kuzunguka nyota za Charles's Wain .