中国国际广播电台
Zhou ni enzi ya tatu baada ya
enzi ya Xia na Shang nchini
China katika zamani za kale.
Enzi ya Zhou, ambayo ilidumu
kwa miaka zaidi ya 770, ilianzishwa
mwaka 1027 kabla ya Kristu na
kuangushwa na nchi ya Qing mwaka
256 kabla ya Kristu. Kabla ya
mji mkuu kuhamia kwa upande
wa mashariki, nchi hiyo iliitwa
kuwa Zhou ya magharibi, na kuitwa
Zhou ya mashariki baada ya mji
mkuu wa nchi kuhamia kwa upande
wa mashariki. Enzi ya Zhou ya
mashariki iligawanyika katika
vipindi viwili vya Chunqiou
na Zhanguo.
Baada ya mji mkuu kuhamia
mji wa Gao ulioko sehemu ya
mashariki, mfalme wa kwanza
wa enzi ya Zhou aliyejulikana
kwa Wu aliongoza majeshi kushambulia
enzi ya Shang na kuasisi enzi
ya kifalme ya Zhou.
Mwaka 770 wa kabla ya Kristu
hadi mwaka 476 wa kabla ya
Kristu ilikuwa enzi ya Chunqiu.
Pamoja na ongezeko la idadi
ya watu na maendeleo ya uchumi,
yalizushwa mapigano makali
ya kugombea umiliki kati ya
nchi kubwa. Hali ya jamii
ilitokewa na mabadiliko makubwa.
Katika uzalishaji wa kilimo,
wakulima walianza kutumia
vyombo vya kilimo vilivyotengenezwa
kwa chuma, kutumia ng’ombe
kulima mashamba na kujenga
miradi ya maji, hatua hiyo
iliongeza uzalishaji wa mazao
ya kilimo. Chunqiu ni kipindi
cha mpito ambapo utaratibu
wa jadi wa kisiasa na kijamii
wa Zhou ya magharibi ulisambaratika
hatua kwa hatua.
Confucius, ambaye alikuwa
mwana nadharia mkubwa na mwanaelimu
mkubwa nchini China, alizaliwa
katika kipindi cha mwisho
cha Chunqiu. Kwenye msingi
wa kujumlisha utamaduni na
mawazo ya zamani, Confucius
akifikiria hali halisi ya
jamii yenye mgogoro, alitoa
mfumo wa maoni ya nadharia
kuhusu utu, uadilifu na masuala
ya kijamii na kisiasa, na
kuanzisha kundi la wasomi
wenye mawazo ya confucius
katika zamani za kale.
Kipindi cha Zhanguo (toka
mwaka 403 kabla ya Kristu
hadi mwaka 221 kabla ya Kristu)
ni kipindi ambacho watawala
wa sehemu mbalimbali nchini
waligombea madaraka baada
ya Zhou ya mashariki. Katika
kipindi hiki, mabadiliko makubwa
yalitokea nchini China: nchi
nyingi ndogo ndogo zilimezwa
na nchi kubwa na hatimaye
zikabaki nchi 7 kubwa. Katika
kipindi hicho, nchi mbalimbali
zilifanya mageuzi, hususan
nchi ya Qin.
Ingawa katika kipindi cha
Zhanguo zilitokea vita mwaka
hadi mwaka, lakini hali hiyo
haikuathiri maendeleo ya utamaduni
wa kale nchini China, shughuli
za kundi la watu wenye elimu
kubwa walistawisha utamaduni
wa fani maalumu. Katika kipindi
hicho utamaduni wa mawazo
ulifikia kileleni katika historia
ya kale ya China yakiwemo
makundi ya Confucius na Menfucius;
kundi la kidao lililowakilishwa
na Laozi, Zhuangzi na Liezi;
kundi la wanasheria lililowakilishwa
na Hanfei; na kundi la Mozi,
makundi hayo yaliungwa mkono
na kuheshimiwa na vizazi vya
baadaye. Hali ya kuweko kwa
makundi yenye mawazo tofauti
yalihimiza maendeleo ya siasa
na uchumi kwa wakati ule,
tena inaendelea hadi hivi
sasa.
Mwaka 230, mfalme Yingzheng
wa enzi ya Qin akitumia muda
wa miaka 9 aliangusha nchi
nyingine 6 na kuunganisha
sehemu zote za China katika
mwaka 230 kabla ya Kristu.
Hadi hapo hali ya mfarakano
uliodumu kwa karibu miaka
600 ilimalizika.
|