中国国际广播电台
Mwaka 206 kabla ya Kristu hadi
mwaka wa 8 ni kipindi cha enzi
ya Han ya magharibi katika historia
ya China. Liu Bang ambaye aliyekuwa
mfalme Gao aliasisi enzi ya
Han na kuchagua Changan kuwa
mji mkuu.
Katika miaka ambayo mfalme
Hangaozu alikuwa madarakani,
aliimarisha utawala wa serikali
kuu na kubuni sera za kuboresha
maisha ya wananchi. Mwaka
159 kabla ya Kristu, mfalme
Hangaozu alifariki, Hui alirithi
ufalme wake, lakini wakati
ule madaraka ya serikali,
yalikuwa mkononi mwa malkia
Lu, ambaye ni mke wa mfalme
Hangao. Malkia Lu alitawala
kwa miaka 16, na ni mmoja
wa watawala wachache wa wanawake
katika historia ya China.
Mwaka 183 kabla ya Kristu,
Wen alirithi ufalme, yeye
na mtoto wake ambaye alirithi
ufalme (toka mwaka 156 kabla
ya Kristu hadi mwaka 159 kabla
ya Kristu) waliendelea kutekeleza
sera za kuboresha maisha ya
wananchi, kupunguza kodi na
kukuza uchumi wa nchi.
Kutokana na sera bora za
wafalme wa hao, nguvu ya enzi
ya Han iliimarika. Mwaka 141
kabla ya Kristu Wu alirithi
ufalme na kutuma Wei Qing
na Huo Qubing kwenda kupigana
vita na kabila la waxiongnu,
hatimaye walishinda vita na
kupanua ardhi ya enzi ya Han
ya magharibi, na kufanya uchumi
na utamaduni kupata maendeleo
katika sehemu ya kaskazini.
Kutokana na kutekelezwa kwa
sera za kukuza uzalishaji
mali na kuboresha maisha ya
wananchi, nguvu ya enzi ya
Han iliimarika, lakini katika
wakati huo huo, nguvu ya mikoa
pia iliimarika ha kuhatarisha
utawala wa kifalme. Mwaka
wa 8 baada ya Kristu, Wang
Mang alijinyakulia ufalme
na kuasisi enzi ya Xin.
Enzi ya Han ya magharibi
ni moja ya enzi yenye nguvu
kubwa katika historia ya China,
hivyo enzi ya Han ilikuwa
katika hali ya utulivu kwa
miaka yote ya utawala wake.
Mfalme Wu alisikiliza pendekezo
la waziri Dong Zhognshu la
“kuacha nadharia nyingine
na kuheshimu nadharia ya Confucius
peke yake.” Tokea hapo, nadharia
na elimu ya Confucius vikawa
sera za kutawala kwa enzi
zote zilizofuata.
Tokea mwaka 25 hadi mwaka
220 ni kipindi cha enzi ya
Han ya mashariki, ambayo iliasisiwa
na Liu Xiu ambaye alijiita
mfalme Guangwu.
Katika miaka ya mwanzo ya
enzi ya Han ya mashariki,
utawala wa serikali kuu uliimarisha
maelewano na utawala wa kikanda,
utawala wa nchi ulielekea
hali ya utulivi, kiwango cha
uchumi, utamaduni, sayansi
na teknolojia kilizidi kile
cha enzi ya Han ya magharibi.
Mwaka 105 Cai Lun alivumbua
teknolojia ya utengenezaji
wa karatasi. Katika upande
wa sayansi ya kimaumbile,
Zhang Heng alivumbua zana
za kuchunguza hali ya sayari
na tetemeko la ardhi. Katika
kipindi cha mwisho cha enzi
ya Han ya mashariki, dakatari
Hua Tuo alifanya upasuaji
kwa wagonjwa kwa kutumia dawa
ya nusukaputi.
|