中国国际广播电台
Kipindi cha Wei na Jin (mwaka
220 hadi mwaka 589) mwishoni
mwa karne ya 2, utawala wa Han
ya mashariki ulizorota, historia
ya China iliingia kipindi cha
muda mrefu cha mfarakano. Mwanzoni
ni nchi tatu zilizokabiliana
za Wei, Shu na Wu (mwaka 189
hadi mwaka 265), hali hiyo ya
kukabiliana ilimalizwa na Jin
ya magharibi, lakini umoja wa
Jin ya magharibi ulidumu kwa
muda mfupi (mwaka 265 hadi mwaka
316), hali ya mfarakano ikatokea
tena. Jamaa za mfalme wa Jin
ya magharibi walianzisha nchi
ya Jin ya mashariki (mwaka 317
hadi mwaka 420), mgogoro wa
mapigano ulitokea katika sehemu
ya kaskazini, ambapo zilianzishwa
nchi 16.
Katika kipindi hicho, uchumi
wa sehemu ya kusini ulikuwa
na maendeleo makubwa. Makabila
yaliyokuwa katika sehemu za
magharibi na kaskazini yalihamia
sehemu ya kati kwa mfululizo,
ambapo uhamiaji na kuishi
kwa kuchanganyika pamoja vilihimiza
kuungana na kuingiliana. Katika
upande wa utamaduni, elimu
kuhusu uhai ilienea kwa haraka,
ambapo dini za kibudha na
kidao zilikuzwa katika mgongano,
lakini kwa kawaida watawala
walilinda dini ya kibudha.
Katika upande wa fasihi na
sanaa kulikuwa na maandishi
na mashairi mengi, michoro
ya sanaa iliyoko katika mapango
ya mawe ya Denghuang ni sanaa
murua ya kudumu.
Katika upande wa sayansi
na teknolojia, Zu Chongzhi
alikuwa mtu wa kwanza aliyefanya
hesabu kuhusu ulinganifu kati
ya mzingo wa duara na urefu
wa kipenyo hadi tarakimu 7
nyuma ya nukta (3.1415926).
Katika kipindi cha enzi za
kusini na kaskazini, uchumi
ulikuzwa zaidi katika sehemu
ya kusini, kwa kuwa watu walioishi
sehemu ya kati walihamia sehemu
ya kusini kwa kujiepusha na
vita, hali ambayo si kama
tu iliongeza nguvukazi ya
sehemu ya kusini, bali pia
ilihimiza sana maendeleo ya
uchumi ya sehemu ya kusini
kutokana na kuingia huko kwa
teknolojia ya kisasa.
Katika kipindi hicho, maingiliano
na nchi za nje yaliendelezwa
kwa nguvu na kufikia hadi
Japan, Korea kwa upande wa
mashariki, Asia ya kati na
Rome kwa upange wa magharibi
na kufikia sehemu ya Asia
ya kusini mashariki.
Ingawa maendeleo ya uchumi
yalikwama katika enzi za sehemu
ya kusini na enzi za sehemu
ya kaskazini, lakini kutokana
na utawala wa makabila yaliyotoka
nje, makabila yaliyoko katika
sehemu ya kati yaliungana
pamoja,. Katika hali ya namna
hiyo, makabila mengine yaliyotoka
sehemu ya kaskazini yaliunganishwa
na kabila la wahan na kuwa
kabila moja. Hivyo, mfarakano
wa enza za kusini na kaskazini
ulifanya kazi muhimu ya kuunganisha
makabila ya China, na ni moja
ya sehemu muhimu ya maendeleo
ya China.
|