中国国际广播电台
Tangu Yang Jian ambaye alikuwa
ni mfalme kuasisi enzi ya Sui
mwaka 581, hadi Yang Guang ambaye
alikuwa mfalme Yang aliponyongwa
mwaka 618, enzi ya Sui ilidumu
kwa miaka 37 tu. Mchango aliotoa
mfalme Wen ulikuwa mkubwa zaidi
ambao ni pamoja na kubatilisha
utaratibu wa zamani wa enzi
ya Zhou ya kaskazini, kubuni
sheria mpya ambayo siyo yenye
adhabu kali kama ya enzi ya
Nanbei.
Tangu kuanzishwa enzi ya
Tang mwaka 618 hadi enzi hiyo
kuangushwa na Zhu Wen mwaka
907, enzi ya Tang ilidumu
kwa miaka 289. Enzi ya Tang
inagawanyika katika vipindi
viwili kutokana na uasi wa
Anshi. Katika kipindi cha
kwanza enzi ya Tang ilistawi,
na katika kipindi cha pili
Tang ilizorota. Tanggaozu
aliasisi enzi ya Tang, lakini
Li Shimin ambaye alikuwa mfalme
Tangtaizong aliongoza jeshi
kuunganisha nchi nzima kwa
kutumia miaka kumi. Baada
ya kutokea uasi wa Xuanwumen,
Li Shimin alikuwa mfalme,
baada ya juhudi kubwa, enzi
ya Tang ilistawi kuliko enzi
zote za China, na iliongoza
duniani katika siasa, uchumi
na utamaduni. Lakini ilipofika
kipindi cha mfalme Tangxuanzong
licha ya kutokea hali ya ustawi
vilevile ilianza kuzorota
baada ya kutokea uasi wa Anshi.
Katika kipindi cha mwisho,
siasa ya enzi ya Tang ilijaa
ufisadi, uasi ulitokea huku
na huku, hatimaye ulitokea
uasi mkubwa wa Huang Chao,
mmoja wa kiongozi aliyeongoza
uasi huo Zhu Wen alijisalimisha
kwa enzi ya Tang, na hapo
baadaye alinyakua madaraka
ya utawala wa enzi ya Tang
na kuwa mfalme, aliasisi enzi
ya Liang ya kipindi cha pili.
|