中国国际广播电台
Mwaka 960, Zhao Kuangyin aliongoza
uasi wa kijeshi na kuasisi utawala
wa Song, ambao uliodumu kwa
miaka 319 na uliangushwa na
enzi ya Yuan mwaka 1279. Enzi
ya Song ilipitia vipindi viwili
vya Song ya kaskazini na Song
ya kusini. Katika wakati huo
huo, watu wa kabila la Qidan
waliasisi nchi ya Liao ambayo
ilidumu kuanzia mwaka 947 hadi
mwaka 1125; Watu wa kabila la
Dangxiang waliasisi nchi ya
Xia ya magharibi (1038-1227)
kwenye sehemu ya kaskazini magharibi
ya enzi ya Song; Mwaka 1115
watu wa kabila la Nuzhen walianzisha
nchi ya Jin (1115-1234) katika
sehemu ya kaskazini. Mwaka 1125
nchi ya Jin ilimeza nchi ya
Liao, na katika mwaka 1127 iliteka
Kaifeng, mji mkuu wa enzi ya
Song na kuwateka nyara wafalme
wa Hui na Qin. Zhaogou wa enzi
ya Song alichukua wadhifa wa
ufalme katika Henan, hapo baada
ye alitorokea Linan, ambayo
hivi sasa inajulikana kwa Hangzhou
iliyoko sehemu ya kusini, na
kuasisi enzi ya Song ya kusini.
Enzi ya Song ya kaskazini
baada ya kuunganisha sehemu
za kaskazini, yalikuwa na
maendeleo makubwa katika jamii,
uchumi, utamaduni pamoja na
biashara na nje baada ya nchi
ya Jin kuangusha utawala wa
Song ya kaskazini, Song ya
kusini ilikalia sehemu ya
kusini ambayo haikuwa na wazo
la kushambulia sehemu ya kaskazini
na kuunganisha upya sehemu
ya kaskazini.
Katika kipindi hiki yalipatikana
maendeleo makubwa katika sayansi
na teknolojia hususan kuvumbua
dira, teknolojia ya uchapishaji
na baruti. Teknolojia iliyovumbuliwa
na Bishen ya uchapishaji kwa
kutumia chapa za neno moja
moja ilitangulia kwa miaka
400 kuliko ile teknolojia
ya Ulaya. Mbali na hayo, katika
upande wa utamaduni walijitokeza
wananadharia pamoja na kuenezwa
kwa dini za kidao, kibudhaa
pamoja na dini zilizotoka
nchi za nje. Katika fasihi,
walijitokeza waandishi wakubwa
wa vitabu pamoja na maandishi
na michoro mashuhuri.
|