中国国际广播电台
Tiemuzhen wa Mongolia aliasisi
nchi yake mwaka 1206, ambayo
ilipewa jina la Yuan na mfalme
Hubilie mwaka 1271. Enzi ya
Yuan iliiangusha enzi ya Song
mwaka 1279 na kuuchagua mji
wa Daou, ambao ni Beijing kwa
hivi sasa, kuwa mji mkuu wake.
Mwanzoni kabisa kabila la
wamongolia lilikuwa katika
sehemu ya kaskazini ya jangwa
kubwa, Tiemuzhen alishinda
makabila yote madogo madogo
ya huko na kuazisha nchi ya
Mongolia, naye akajiita kuwa
mfalme Chengjisihan. Kabla
ya hapo jeshi la Mongolia
liliishambulia sehemu ya magharibi
hadi Asia ya kati, Ulaya ya
mashariki na Uajemi. Nchi
hiyo kubwa, ambayo kitovu
chake ni Jamhuri ya Watu wa
Mongolia ya hivi sasa ilifarakana
na kugawanyika kuwa nchi kadhaa
za kifalme, ambazo kwa jina
zilikuwa chini ya mfalme wa
Chengjisihan.
Katika enzi ya Yuan, nchi
zilizokuwa sehemu ya kaskazini
zilipigana vita kwa miaka
mingi na kuleta uharibifu
mkubwa. Mfalme wa kwanza wa
enzi ya Yuan aliweka kipaumbele
katika kilimo na kurekebisha
mto Manjano.
Katika enzi za Tang, Song
na Yuan China ilikuwa nchi
iliyoendelea kabisa duniani,
ambayo uchumi na utamaduni
vilivutia sana nchi jirani.
Katika kipindi kile mabalozi,
wafanyabiashara na wasomi
wengi wa nchi za mashariki
na magharibi walitembeleana,
na uhusiano wa kidiplomasia
kati ya China na nchi za nje
ulikuzwa kwa haraka. Nchi
ya Yuan ilikuwa na uhusiano
mkubwa na Japan pamoja na
nchi za Asia ya kusini mashariki,
na kwenye bahari merikebu
(mashua kubwa) nyingi za China
zilikuwa zikisafiri kati ya
China na India. Uvumbuzi mkubwa
tatu za uchapaji, baruti na
dira zilienezwa hadi Ulaya
kwa kupitia Uarabu katika
enzi ya Yuan. Elimu ya sayari,
tiba na hisabati ziliingia
China na dini ya kiislamu
ilienezwa katika China. Mawasiliano
kati ya China na peninsula
ya uarabuni licha ya kupitia
baharini kulikuwa na njia
ya kupitia mkoa wa Yunan kwenye
nchi kavu, ambapo vyombo vya
kauri vya China vilisafirishwa
hadi Afrika ya mashariki hata
nchini Morocco. Mwaka 1275,
mtoto wa mfanyabiashara mashuhuri
wa Venice alifuatana na babake
walifika China na kuishi kwa
miaka 17, kitabu walichoandika
kijulikanacho kwa “kumbukumbu
ya matembezi” kilikuwa kitabu
muhimu kuhusu kuifahamu China
na Asia kwa watu wa nchi za
magharibi katika karne kadhaa.
Katika upande wa utamaduni,
walijitokeza watungaji wa
michezo ya opera wakiwa ni
pamoja na Guan Hanqing, Wang
Shipu, Bai Pu na Ma Zhiyuan.
Utawala wa Mongolia uliwakandamiza
sana watu wa kabila la wahan,
ambao ulisababisha upinzani
mkubwa. Mwaka 1333, wakulima
waliounganishwa kwa shughuli
za kidini na jumuiya mbalimbali
walifanya uasi sehemu mbalimbali
nchini. Mwaka 1351 wakulima
waliopelekwa kurekebisha mto
Manjano walifanya uasi mkubwa
wakijitambulisha kwa kufunga
skafu nyekundu vichwani. Mwaka
1341 jeshi la “skafu nyekundu”
liliangusha utawala wa Yuan
na kuanzisha enzi ya Ming.
|