中国国际广播电台
Mbinu
za kijeshi za Sunzi ni maandiko
makubwa mashuhuri ya kele
ya China kuhusu nadharia ya
kijeshi, na ni moja ya maandishi
yenye athari kubwa zaidi na
kuenezwa kwenye maeneo makubwa
zaidi duniani. Mawazo ya mbinu
na falsafa iliyoko kwenye
maandiko hayo yanatumika sana
katika maeneo mbalimbali yakiwemo
ya kijeshi, kisiasa na kiuchumi.
Kitabu cha “Mbinu za Kijeshi
za Sunzi” kiliandikwa miaka
2,500 iliyopita na ni maandiko
ya nadharia ya kijeshi cha
mapema zaidi duniani, ambayo
ni mapema kwa miaka 2,300
kuliko kitabu cha “On War”
kilichoandikwa na Clausewitz
wa Ulaya.
Mwandishi wa kitabu cha “Mbinu
za Kijeshi za Sunzi” ni Su
Wu ambaye alikuwa bingwa wa
kijeshi katika kipindi cha
Chunqiu na kuheshimiwa kuwa
“mwanaelimu mkuu wa kijeshi”
katika kipindi cha Chunqiu.
Wakati ule Sun Wu ili kukwepa
vita alikimbilia nchi ya Wu
na kuteuliwa kuwa jemadari
wa mfalme wa Wu, alishinda
jeshi lenye askari laki 2
la nchi ya Chu kwa kutumia
jeshi lake lenye askari elfu
30. Sun Wu alijumlisha uzoefu
wa kivita hadi miaka ya mwisho
ya kipindi cha Chunqiu na
kutoa mfumo kamili wa nadharia
ya mambo ya kijeshi. Kitabu
cha “Mbinu za Kijeshi za Sunzi”
kina maneno zaidi ya 6,000
na chenye makala 13, ambazo
kila makala inaeleza mada
moja. Wazo la kitabu hicho
ni njia bora zaidi katika
mambo ya kijeshi ni kupata
ushindi kwa kutumia mbinu
za kisiasa, halafu ni mbinu
za kidiplomasia, za kutumia
nguvu za kijeshi na mwisho
ni kuteka mji wenye ngome.
Hivyo bingwa wa kivita anapaswa
kujua yali halisi za adui
na kupata habari kwa kutumia
majasusi. Kitabu cha “Mbinu
za Kijeshi za Sunzi” ni chenye
mawazo ya kifalsafa. Kwa mfano
maneno ya “Ukijua hali halisi
zako na za adui, utashinda
daima” sasa yanatumiwa hata
na watu wa kawaida. Kitabu
hicho cha “Mbinu za Kijeshi
za Sunzi” kimechapishwa kwa
lugha za aina 29 zikiwemo
za Kingereza, Kirusi, Kijerumani
na Kijapan. Vyuo vya nchi
nyingi duniani vinatumia kitabu
cha “Mbinu za Kijeshi za Sunzi”
kama kitabu chao cha kiada.
Habari zinasema kuwa katika
vita vya ghuba mwaka 1991,
pande mbili zilizopigana zote
zilifanya uchunguzi juu ya
kitabu cha “Mbinu za Kijeshi
za Sunzi”. Hivi sasa mawazo
ya kitabu hicho yanatumiwa
sana katika sekta nyingi zikwemo
za kijamii na kibiashara.
|