Kitabu cha Historia
中国国际广播电台

“Kitabu cha Historia” ni maandishi makubwa ya historia ya China, ni maandishi makubwa ya fasihi ya kuandika watu na mambo halisi, na kulikuwa na athari kubwa kwa elimu ya historia na fasihi kwa vizazi vilivyofuta vya China. “Kitabu cha Historia” kiliandikwa na Si Maqian katika enzi ya Han ya magharibi, karne ya kwanza kabla ya Kristu kuhusu mambo yaliyotokea katika miaka 3,000 iliyopita ya maeneo ya siasa, uchumi, utamaduni na historia tangu zamani za kale hadi enzi ya Han ya magharibi. Kitabu hicho alichoandika Si Maqian kwa miaka 13, kina makala 103 zenye maneno ya kichina zaidi ya laki 5, mambo aliyoandika ni pamoja na elimu ya sayari, kalenda, miradi ya maji, uchumi na utamaduni; shughuli na mambo kuhusu koo za kifalme na mabwenyenye za enzi mbalimbali; na mambo kuhusu watu mashuhuri wa enzi mbalimbali na historia ya makabila madogomadogo. “Kitabu cha Historia” kiliandika mambo halisi wala siyo kama vitabu vitatu walivyoandika maofisa wa historia wa enzi mbalimbali, ambavyo viliandika mafanikio tu na kusifu wafalme na mawaziri wao.