中国国际广播电台
Katika historia ndefu ya kimwinyi
yenye miaka zaidi ya 2,000 vilitokea
vipindi kadhaa vyenye ustawi,
ambavyo ni pamoja na kipindi
cha “Wenjing” cha enzi ya Han
ya magharibi, kipindi cha “Zhenguan”
cha enzi ya Tang, kipindi cha
“Yongxuan” cha enzi ya Ming,
kipindi cha “Kangyong” cha enzi
ya Qing pamoja na kipindi ambacho
watu wengi hawakijui cha “Zhangguo”.
Kila kipindi chenye ustawi
kina umaalumu wa namna moja,
yaani sehemu zote zimeunganishwa
kama kitu kimoja, uchumi unastawi,
siasa vimetulia, jamii yenye
amani na usalama, nguvu ya
nchi imeimarika na utamaduni
umeendelezwa vizuri.
Katika kipindi cha Chunqiu
utaratibu ulivurugika, Confucius
alikichukulia kuwa ni kipindi
chenye vurugu, lakini mambo
yalionesha kuwa utaratibu
wa zamani utaangamia na utaratibu
mpya utatokea. Baada ya kuingia
kipindi cha Zhanguo, Lili
na Wuqi walifanya mageuzi
kwa mbalimbali katika nchi
ya Wei na nchi ya Chu. Ilipofika
miaka ya kati na mwisho ya
kipindi hicho nchi za Qin,
Han, Qi, Zhao na Yan ziliimarika
kutokana na mageuzi, hususan
ni kuwa Sangyang alifanya
mageuzi makbuwa zaidi katika
nchi ya Qin, hatimaye nguvu
ya Qin ilikuwa kubwa zaidi
kuliko nchi nyingine 6. Ingawa
mageuzi yalifanywa kwa viwango
tofauti katika nchi mbalimbali
za kipindi kile, lakini hatimaye
zilimaliza au kimsingi zilimaliza
mageuzi ya utaratibu wa jamii,
na utaratibu wa kitumwa ulibadilishwa
na utaratibu wa kimwinyi.
Nchi ya Qin, ambayo iliteka
nchi nyingine 6, ilitawaliwa
kidikteta na mfalme mmoja,
na ni mara ya kwanza kutimiza
nadharia ya “mungano mkubwa”
uliotarajiwa toka kipindi
cha Chunqiu. Tokea hapo, mungano
na mfarakano ilikuwa moja
ya kanuni inayotumika kuangalia
maendeleo ya jamii. Ni dhahiri
kuwa aina zote za mungano
ni sahihi na aina zote za
mfarakano ni makosa. Wakati
nchi fulani ikitawaliwa na
ufisadi, maendeleo ya nguvu
ya uzalishaji mali yamekwamishwa
vibaya au kuzorota, wananchi
wanaishi kwa shida kubwa,
uasi wa wakulima ukafarakanisha
umoja wa nchi hiyo, basi ufarakanishaji
huo ni mzuri na unatakiwa
kufanya hivyo. Hayati Mao
Zedong kupongeza umuhimu wa
uasi wa wakulima wa China
ndiyo kutokana na msingi huo.
Lakini baada ya mfarakano
nchi kwa vyovyote itarejea
katika mungano, hii ni kanuni
ya maendeleo ya historia ya
China, kwani muungano mkubwa
unaleta mazingira tulivu ya
jamii, ambayo yananufaisha
maendeleo ya uzalishaji mali
wa jamii na uboreshaji wa
maisha ya wananchi. Katika
wakati huo kutimiza “mungano
mkubwa” ni sharti kubwa la
kuangalia kipindi cha historia
ni chenye ustawi ua la.
Enzi za Han na Tang, ambazo
“muungano mkubwa”, hivyo ni
vipindi viwili muhimu vya
historia, ambapo eneo la China
lilipanuka.
Kila kipindi chenye ustawi
kilikuwa na mazingira ya “muungano
mkubwa”, kuwa na amani na
usalama, maendeleo ya uzalishaji
mali, nafaka za kutosha na
serikali kuwa na fedha nyingi.
Mfalme Wu wa enzi ya Han alistawisha
nchi kwa miaka zaidi ya 60,
nchi ilikuwa salama na kuwa
na fedha nyingi. Katika miaka
ya mwanzo ya enzi ya Tang,
kila ukoo ulikuwa na akiba
ya nafaka kwa miaka kadhaa.
Katika miaka ya wafalme wa
Yong na Xuan ya enzi ya Ming,
wananchi waliishi maisha ya
neema na nchi ilikuwa na nguvu
kubwa ya kifedha. Katika miaka
ya mfalme Kangxi ya enzi ya
Qing, nchi ilikuwa na akiba
kubwa zaidi, katika miaka
ya 50 tangu Kangxi kuwa mfalme
wa Qing, kodi zilisamehewa
kote nchini kwa wiki moja
katika muda wa miaka 3, wakati
baadhi ya mikoa ilisamehe
au kupunguza kodi kila mwaka.
Qianlong aliporithi ufalme,
Qing ilikuwa na nguvu kubwa
zaidi, mfalme alisamehe kodi
kote nchi kwa mara nne.
|