中国国际广播电台
Baada
a Qinshihuang kuwa mfalme
wa enzi ya Qin, alitawaliwa
na tamaa ya kuwa na maisha
ya kudumu, alipata habari
kuwa kuna mlima kwenye bahari
ya Bo, ambapo kuna dawa zinazoweza
kufanya mtu anayekula dawa
hiyo kutofariki, hivyo alituma
watu kwenda kutafuta dawa
hiyo, lakini hawakuona dawa
hiyo.
Lu Sheng alirudi na mikono
mitupu, mfalme Qinshihuang
akamtuma Xu Fu kwenda kuitafuta
dawa hiyo tena. Xu Fu aliporudi
kutoka baharini alimwambia
mfalme kuwa aliona mlima wa
Penglai na dawa hiyo pia,
lakini viumbe waliokuwa wanaoishi
kwenye mlima huo walimnyima
na kusema kuwa zawadi aliyopeleka
ni kidogo sana, na walisema
kuwa mfalme akitaka dawa hiyo,
sharti awapelekee wanaume,
wanawake na mafundi hodari.
Mfalme alifurahi sana baada
a kusikia kuwa Xu Fu aliona
dawa hiyo, akachagua watoto
elfu 3 wa kike na wa kiume
pamoja na mafundi hodari,
alimtuma Xu Fu kwenda tena
kwenye mlima wa huo. Xu Fu
hakuona dawa hiyo, lakini
aliogopa kurejea na kuonana
na mfalme, hivyo aliongoza
watu hao kwenda Japan na wakaanza
kuishi huko. Hatimaye Xu Fu
alifariki kwenye mlima wa
Fuji nchini Japan.
Nchini Japan kuna hadithi
na maandishi mengi ya kumbukumbu
kuhusu Xu Fu, hata baadhi
ya wanaelimu wanaona kuwa
Xu Fu ndiye mwanzilishi wa
nchi ya Japan, watu wa Japan
vilevile wanamchukulia Xu
Fu kama mtakatifu wa jadi
na kumwabudu.
|