中国国际广播电台
Mapango ya Mogao ni ya kwanza
kwa ukubwa na kamilifu ya mabaki
ya dini ya kibudha duniani.
Hiyo kama bohari ya vitu va
sanaa inayofuatiliwa na watu
wengi duniani, kwa nini ilijengwa
kwenye genge la mlima ulioko
kwenye jangwa la Gobi, sehemu
ya kaskazini magharibi ya China?
Inasemekana kuwa mahali palipochimbwa
mapango ya Mogao huko Denghuang
palichaguliwa na mtawa Yue
Zun. Mwaka 366 Yu Zun katika
matembezi yake alifika chini
ya mlima wa Sanwei, wakati
ule ulishakuwa jioni, lakini
hakupata mahali pa kulala,
alipokuwa akiwaza, ghafla
alinyanyua kichwa na kuona
maajabu kwamba kulikuwa na
mwangaza wa rangi ya dhahabu
kwenye mlima uliotazamana
naye, na kama kulikuwa na
budha walioonekana katika
mwangaza. Yue Zun alishangazwa
sana na kuona kuwa kumbe hapo
ni mahali patakafitu! Hivyo
alitafuta watu kuchimba kwenye
genge la mlima huo, na kulikuwa
na mapango zaidi ya 1,000
ktika enzi ya Tang.
Utafiti uliofanywa na wataalamu
unaonesha kuwa uchimbaji wa
mapango ya mawe ya Mogao ni
mafanikio ya akili ya mababu
jadi, mapango kuchaguliwa
kuchimbwa kwenye jangwa ni
kutokana na wazo la kuungana
na mazingira ya kimaumbile
na kutengana kati ya dini
ya kibudha ya maisha na desturi
ya binadamu.
|