Mabaki ya Bustani ya Yuanming Yako Wapi
中国国际广播电台
Mwaka 1860 jeshi la mungano la Uingereza na Ufaransa lilivamia Beijing na kuingia bustani ya Yuanming, walichukua kila kitu chenye thamani. Vitu vya zawadi lilivyotoa jeshi la Ufaransa kwa mfalme wake baada ya kurejea nchini vilikuwa karibu elfu 10. Hivi sasa watu wakitaka kuona vitu vilivyokuwako katika bustani ya Yuanming hawana budi kwenda nchini Uingereza na Ufaransa.

   Katika Jumba la Makungusho la Uingereza mjini London vinaoneshwa vitu vyenye thamani elfu makumi kadhaa vilivyochukuliwa kutoka bustani ya Yuanming. Mfalme Napoleon wa tatu wa Ufaransa alijenga ‘Jumba la China” katika boma moja maarufu la nchini Ufaransa kwa kuonesha vitu zaidi ya elfu moja vya utamaduni vya China.