中国国际广播电台
Visukuku
vya sokwe-mtu wa Beijing kabla
ya kupotea vilihifadhiwa katika
sanduku la chuma la usalama
la hospitali moja ya mji wa
Beijing.
Siku chache kabla ya kuzuka
vita ya Pasifiki, profesa
Wei Dunrui, ambaye ni mtaalamu
mashuhuri wa utafiti wa visukuku
hivyo, aliona kuwa hospitali
hiyo haikuwa mahali salama
tena, hivyo alipendekeza kuvipeleka
na kuhifadhiwa visukuku hivyo
nchini Marekani. Siku moja
ya wiki 2 au 3 kabla ya kuzuka
tukio la Pearl Harbor, ofisa
wa idara ya huduma ya hospitali
hiyo Bo Wen aliarifu kuviweka
visukuku 147 yakiwemo mafuvu
5 katika masanduku mawili
ya mbao na kuyasafirisha hadi
kwenye ubalozi wa Marekani
mjini Beijing ili yasafirishwe
pamoja na askari wa Marekani
hadi Marekani. Lakini tokea
hapo visukuku hivyo vilipotea
na hakuna habari yoyote kuhusu
visukuku hivyo.
Katika miaka ya karibuni,
mtaalamu kuhusu elimu ya binadamu
Bw. Zhou Guoxing alisikia
kuwa siku chache kabla ya
kusuka tukio la Pearl Harbor,
askari mmoja aliyelinda mlango
kati ya makao makuu ya jeshi
la baharini la Marekani na
ofisi ya ubalozi wa Marekani,
aliona watu wawili walikuwa
wakibeba sanduku moja na kulifukia
katika ua ulioko sehemu ya
nyuma ya nyumba ya ofisi ya
ubalozi, na alikisia kuwa
vitu vilivyokuwemo ndani ya
sanduku hilo vilionekea kuwa
ni visukuku vya sokwe-mtu
wa Beijing. Bw. Zhou Guoxing
alifika hapo, lakini hakuweza
kuchimba, kwani sehemu hiyo
imejengwa nyumba. Visukuku
hivyo vilipotea kabla ya miaka
miongo kadhaa iliyopita na
hakuna habari yoyote kuhusu
vitu hivyo. Hayati Zhou Enlai
alipokuwa hai aliwahi kusema
kuwa ni wachina kadhaa, ambao
walikabidhi visukuku vya sokwe-mtu
kwa wamarekani na vilipotea
mikononi mwa wamarekani, wanasayansi
waadilifu wangevirudisha kwa
China.
|