Habari zisizofahamika kuhusu Yang Yuhuan
中国国际广播电台
 

Yang Yuhuan alikuwa mke mdogo wa mfalme Li Mao ambaye ni mtoto wa mfalme Tang Xuanzong, hapo baadaye alipendwa na Tang Xuanzong na kuwekwa katika jumba la kusini la mfalme. Baadaye Yang Yuhuan alithibitishwa kuwa mke mdogo wa mfalme Tang Xuanzong na kuishi kama malkia. Wakati ule mfalme Tang Xuanzong alikuwa na umri wa miaka 56 na Yang Yuhuan alikuwa na umri wa miaka 22.

Yang Yuhuan alikuwa ni kisura na mnene kiasi, alikuwa anafahamu sana muziki, kucheza ngoma na namna ya kumfurahisha mfalme, hivyo alipendwa sana na mfalme Tang Xuanzong.

Kutokana na Yang Yuhuan kupendwa na mfalme Tang Xuanzong, jamaa zake wote walinufaika sana kutokana naye. Baadhi ya ndugu zake walikuwa maofisa hata mmoja wao alikuwa waziri mkuu ambaye alijitwalia madaraka makubwa. Mfalme alipenda sana wanawake, kunywa pombe na kuponda raha, hatimaye ukatokea “uasi wa Anshi”. Mfalme Tang Xuanzong hakuwa na la kufanya ila tu alimtaka Yang Yuhuan ajiue.

Kuhusu kifo cha Yang Yuhuan kuna misemo ya aina nyingi. Baadhi ya watu wanasema kuwa Yang Yuhuan hakufa, mtu aliyekufa ni mwanamke mmoja aliyefanana naye. Mtafiti wa kitabu cha hadithi maarufu cha “Ndoto kwenye Jumba Jekundu” Bw. Yu Pingbo alisema kuwa yule aliyejinyonga alikuwa ni msichana mtumishi wa mfalme, lakini Yang Yuhuan alikimbilia Japan.

Mwaka 1963 kulikuwa na msichana mmoja wa Japan ambaye alionesha nasaba kuhusu ukoo wake na kusema kuwa yeye ni kizazi cha Yang Yuhuan. Nyota wa filamu ya sinema wa Japan msichana Momoe Yamaguchi pia alijidai kuwa ni kizazi cha Yang Yuhuan.

Nchini Japan pia kuna misemo ya aina nyingi. Mmoja wa misemo hiyo unasema kuwa yule aliyekufa alikuwa mwanamke aliyefanana na Yang Yuhuan, lakini Yang Yuhuan mwenyewe alikimbilia kijiji kimoja nchini Japan.

Baada ya kutuliza “uasi wa Anshi” mfalme Tang Xuanzong alituma mtu kwenda Japan kumtafuta Yang Yuhnan, Yang Yuhuan alikabidhiwa sanamu mbili za budhaa alizotoa mfalme Tang Xuanzong, na Yang Yuhuan alitoa pambo moja la kichwani kama zawadi kwa mfalme. Sanamu hizo mbili hadi hivi sasa bado zinahifadhiwa nchini Japan, mahali alipozikwa Yang Yuhuan. Mbele ya kaburi la Yang Yuhuan kuna mbao mbili zenye maelezo, moja ni kuhusu kaburi na nyingine ni kuhusu Yang Yuhuan. Wajapan wanapenda kutoa heshima kwenye kaburi la Yang Yuhuan, wakiona kuwa kufanya hivyo wataweza kuzaa mtoto mzuri. Hivi sasa serikali ya Japan inafikiria kufanya kaburi la Yang Yuhuan kuwa sehemu moja ya utalii kwa watu.