Habari kuhusu njia ya hariri
中国国际广播电台
Njia ya hariri ni njia muhimu ya kuenea kwa ustaarabu wa kale wa China kwa nchi za magharibi, na ni daraja la maingiliano ya uchumi na utamaduni kati ya China na nchi za magharibi.
Njia ya hariri inaanzia mji wa Changan kwa upande wa mashariki hadi Rome kwa upande wa magharibi, njia hiyo ina matawi mawili, ambayo njia ya kusini omatpla Denghuang kupitia Xinjiang na Afghanistan, Iran, peninsula ya Uarabu hadi nchi ya Rome. Njia ya kaskazini inatoka Denghuang, kupitia sehemu ya Asia ya kati ya Russia kisha inaelekea upande wa kusini magharibi na kuungana na njia ya ile ya kusini. Njia zote mbili zinajulikana kama ni “njia za hariri ardhini”.
Aidha, kuna njia mbili za hariri ambazo watu wengi hawazifahamu. Moja ya njia hiyo inajulikana kwa j9na la “njia ya hariri ya kusini magharibi”. Njia hiyo inatoka mkoa wa Sichuan, kupitia mto wa Yiluowadi, Menggong iliyoko sehemu ya kaskazini ya nchi ya Myanmarr, baada ya kuvuka mto wa Qindun, inafikia Nepal iliyoko sehemu ya kaskaizni mashariki ya India, kisha inafuata mto wa Ganges, kisha inapitia sehemu ya kaskazini magharibi ya India na kufika kwenye uwanda wa juu wa Iran. Njia hiyo ya hariri ilikuweko mapema zaidi kuliko zile za ardhini.
Njia nyingine ya hariri inatoaka mji wa Guangzhou, kupitia mlango bahari wa Malacca, Sri lanka, India hadi Afrika ya mashariki. Njia hiyo inajulikana kwa “njia ya hariri ya baharini”. Mabaki ya kale yaliyofukuliwa kutoka baadhi ya sehemu za Afrika mashariki ikiwemo Somalia, yanathibitisha kuwa njia hiyo ya hariri ilianzishwa katika enzi ya Song ya China.
“Njia ya hariri ya baharini” iliunganisha nchi muhimu za asili ya ustaarabu na sehemu za chanzo cha utamaduni duniani, ambazo zinahimiza maingiliano ya uchumi na utamaduni ya katika sehemu hizo, hivyo inaitawa kuwa ni “njia ya mazungumzo kati ya mashariki na magharibi. Kitabu cha historia kinasema kuwa msafiri Maco Polo hapo zamani alifika China kwa kupitia “Njia ya hariri ya baharini”. Wakati aliporejea nyumbani pia alipanda marikebu kutoka Quanzhou ya mkoa wa Fujian na kuridi Venice, Italia.