Katika historia, Taiwan iliwahi
kuitwa kuwa Yizhou, Dongfan
na Dayuan. Hapo baadaye watu
waliita Taiwan kuwa “Kisiwa
cha Hazina” kutokana na kuwa
na rasilimali nyingi, “Kisiwa
cha matufaha pori ya kichina”
(umbo lake linafanana na majani
yake), “Kisiwa cha Spring” (hali
ya hewa yake si joto wala baridi),
“Kisiwa cha Vipepeo” (kuna vipepeo
wengi), kisiwa cha marijani
(kuna marijani nyingi), na “Kisiwa
cha Sukari” (kuna miwa mingi).
Wakoloni wa Ulaya waliwahi kuita
Taiwan kuwa “Farmosa” (Kisiwa
Kizuri), vilevile waliwahi kuita
Taiwan kuwa “Kisiwa cha Wavuvi”.