Kwa Nini Wachina Wanaitwa “Vizazi Vya Dragon”
中国国际广播电台
Wachina wanaitwa kuwa “vizazi vya dragon”, chanzo chake ni alama na hadithi ya kale. Inasemekana kuwa kabla ya mfalme Huang kulishinda kabila la Ciyou na kuunganisha sehemu za kati za China alichukulia “dubu” kama ni alama yao, lakini baada ya kuliteka kabila la Ciyou ili kufariji maeneo yaliyojisalimisha mfalme Huang aliacha kutumia alama hiyo ya “dubu” na kutumia “dragon” kama ni alama yao mpya, ambayo ni mchanganiko wa kichwa cha “dubu” na mwili wa aina moja ya “nyoka”. Alama ya “dragon” ni mchanganiko wa taswira za jamii za wanaume na wanawake, hali ambayo inaonesha historia ya maendeleo ya taifa na mchakato wa muungano wa makabila mbalimbali ya China.

“Dragon” ikawa alama ya babu za jadi za taifa la China, hivyo taifa la China limehusishwa na “dragon”. Kulikuwa na hadithi inayosema kuwa mfalme Yan ni mtoto wa mwanamke aliyejulikana kwa jina la “Deng” kutokana na kuhurumiwa na mungu wa Dragon wa mbinguni. Maadamu babu jadi wa taifa la China alikuwa kizazi cha “Dragon” wa mbinguni, hivyo vizazi vya taifa la China vilevile ni vizazi vya dragon.