中国国际广播电台
Kila mtu anapewa jina tangu
anapozaliwa, na baadaye atashiriki
katika shughuli za jamii kwa
kutumia jina lake, ambalo linafanya
kazi ya kumwakilisha na kumtofautisha
na watu wengine. Lakini katika
jamii ya China ya kale, majina
yana maana kubwa zaidi.
Katika historia ndefu, utamaduni
wa majina ya wachina ulikuwa
kitu muhimu katika maisha
halisi na maisha ya kiroho
ya taifa la China, na ulifanya
kazi muhimu katika maeneo
ya saisa, utamaduni na jamii.
Data za utafiti wa mabaki
ya kale zinaonesha kuwa zaidi
ya miaka milioni moja iliyopita,
wachina walikuwa wameishi
katika ardhi ya nchi hiyo
ya kale, lakini historia ya
“majina” ilianza katika jamii
ya kiume ya miaka 5,000 au
6,000 iliyopita. Umaalumu
wa jamii ya kike ni kuwa wanawake
walikuwa na hadhi ya kuongoza
katika usimamizi wa shughuli
za ndani za jamii, na kufuata
utaratibu wa kuoana kati ya
koo tofauti, ambapo watu wa
ukoo mmoja ilikuwa ni mwiko
kuoana. Kwa kufuata utaratibu
huo, kulikuwa na haja ya kuchunguza
uhusiano wa watu wa kila jamii,
hivyo yakatokea majina ya
koo ili kuthibitisha uhusiano
wa damu moja.
Utafiti uliofanywa na Gu
Yanwu, mwanachuo mashuhuri
wa enzi ya Qing unaonesha
kuwa zamani za kale nchini
China kulikuwa na majina ya
koo 22, na huenda kulikuwa
na majina mengi zaidi ya koo,
lakini huenda yalizama katika
maji ya mto wa historia, na
yale yaliyoendelea pia yalikuwa
na mabadiliko makubwa. Kabla
ya miaka 4,000 au 5,000 iliyopita,
baada ya kupita katika jamii
ya kike, wachina waliingia
katika kipindi cha jamii ya
kiume, jamii yenye koo mbalimbali
iliingia haraka katika jamii
yenye matabaka ya watu. Moja
ya alama muhimu za kipindi
hicho cha mpito ni kuingiliana
na kupigana kati ya koo zenye
mababu jadi mbalimbali.
Katika karne ya 3 kabla ya
Kristu, enzi ya Qin iliunganisha
sehemu zote za China, ambapo
majina ya koo yaliyotoka katika
jamii ya kike mwanzoni kabisa
yaliungana na majina ya koo
yaliyotoka katika jamii ya
kiume. Tokea hapo katika jamii
ya umwinyi iliyoendelea kwa
miaka zaidi ya 2,000, enzi
zilibadilishwa kwa miongo
kadhaa, na kila badiliko lilipotokea
hutokea maeneo ya ardhi ya
tuzo na kutokea majina mapya
ya koo. Utamaduni wa namna
hiyo ulirithiwa na vizazi
vya baadaye. Wazo kali la
kufuatilia majina ya koo za
babu jadi ni kiini cha umoja
huo. Hadi hivi sasa bado kuna
wachina wanaoishi nchi za
nje ambao wanarejea China
kufuatilia vyanzo vya koo
zao.
|