中国国际广播电台
Inasemekana kuwa malkia Luo
mke wa mfalme Huang aliwafundisha
watu utaalam wa ufugaji wa mafunza
wa hariri miaka zaidi ya 5,000
iliyopita.
Katika enzi ya Han ya magharibi,
Zhang Qian alisafiri kwa upande
wa magharibi na kupeleka vitambaa
vya hariri hadi Ulaya. Watu
wa Ulaya walipoona vitambaa
laini na vya kung’ara walivinunua
haraka.
Mwanzoni watu wa Ulaya hawakujua
vitambaa hivyo vilifumwa kwa
nyuzi zilizotolewa na mafunza
wa hariri, walifikiri kuwa
nyuzi hizo zilitolewa katika
mti fulani, kisha kulainishwa
kwa maji. Baada ya kujua kuwa
vitamba hivyo vilifumwa kutokana
na nyuzi za mafunza wa hariri,
walipania kujifunza utaalam
wa kufuga mafunza wa hariri.
Ilipofika karne ya 6, mfalme
Jadincean wa Rome alionana
na padri mmoja aliyewahi kufika
China na kumtaka aende China
kuiba mbinu ya kufuga mafunza
wa hariri. Padri huyo alifika
Yunnan, China alifahamishwa
maarifa ya kufuga mafunza
wa hariri kwa majani ya miforosadi,
alirejea Rome kwa haraka,
lakini alikanganyika badala
ya kupasha joto mbegu wa mafunza
kifuani mwake alizipanda kwenye
ardhi na kuweka mbegu wa mti
wa mforosadi kifuani mwake
badala ya kuzipanda kwenye
ardhi, hatimaye alishindwa.
Padri huyo alituma mapadri
wengine wawili waende China
kukamilisha kazi hiyo, mapadri
hao wawili walikumbuka sana
fundisho alilopata yule padri
wa kwanza na kuweka maandishi
kuhusu upandaji miti na kupasha
joto mbegu za mafunza wa hariri
katika uwazi wa katikati ya
bakora zao na kurudi Rome.
Tokea hapo maarifa ya ufugaji
wa mafunza wa hariri yaliingia
barani Ulaya.
|