Asili na Mabadiliko ya Maneno ya Kihan
中国国际广播电台


Maneno ya kabila la wahan ni moja ya maneno yaliyotumika kwa miaka mingi, yenye nafasi kubwa ya matumizi na kutumiwa na idadi kubwa sana ya watu duniani. Kuvumbuliwa na kutumika kwa maneno ya kihan, si kama tu kumehimiza maendeleo ya utamaduni wa taifa la China bali pia kumeathiri sana maendeleo ya utamaduni wa dunia.

Zaidi ya miaka 6,000 iliyopita kwenye sehemu yalipo majengo ya Banpo, kulikuwa na aina zaidi ya 50 za michoro, inayoonekana kama ni maandishi ya kawaida, wataalamu wanasema kuwa huenda hiyo ndiyo asili ya maneno ya kihan.
  Maneno ya kihan yalikamilika katika hatua ya mwanzo katika enzi ya Shang karne ya 16 kabla ya Kristu. Katika kipindi cha awali cha enzi ya Sahng, ustaarabu wa China ulifikia kiwango cha juu, na moja ya alama yake ni kuwa na maandishi yaliyochungwa kwenye magamba ya kobe. Katika enzi ya Sahng, mfalme kabla ya kufanya jambo lolote alikuwa huagua, kwa kutumia mabamba ya kobe.

 

Hivi sasa watafiti wa mabaki ya kale wamegundua mabamba ya kobe vipande zaidi ya elfu 160 vyenye maneno zaidi ya 4,000. Maandiko kwenye magamba ya kobe yalikuwa msingi wa maendeleo ya maneno ya kabila la wahan.

Maandiko ya maneno ya kihan, ambayo yanafanana na vitu vyenyewe, yana maneno kiasi cha elfu 10 na yale yanayotumika mara kwa mara ni kiasi cha elfu 3.

Kuvumbuliwa maneno ya kihan kulileta athari kubwa kwa nchi jirani. Maandiko ya kijapan, kivietnam na kikorea yalivumbuliwa kwa msingi wa maneno ya kihan.