Sauti ya Kongele la Yongle Zafikia Umbali wa Kilomita 45
中国国际广播电台

 Katika hekalu ya Dazhong mjini Beijing kuna kengele moja kubwa inayojulikana kwa jina la dazhong. Kengele hiyo, ambayo ilitengenezwa miaka zaidi ya 500 iliyopita, ina uzito wa tani 46.5, kimo cha mita 6.75 na kipenyo cha mita 3.3.

Sauti ya kengele ya Yongle ni nzuri sana, mawimbi ya sauti yake yanalingana na mawimbi ya sanifu ya muziki. Kangele hiyo inapogongwa taratibu, sauti yake ni ndogo na inavutia, na inapogongwa kwa nguvu sauti yake ni kubwa na nene, ambayo inaweza kufikia umbali wa kilomita 45 na sauti hiyo inaendelea kwa dakika zaidi ya 2.


  Kila ifikapo siku ya mwaka mpya, kengele kubwa ya Yongle hugongwa, na desturi hiyo imeendelea kwa miaka zaidi ya 500. Wataalamu wa China walifanya upimaji kuhusu kengele hiyo, waliona kuwa kengele hiyo ilitengenezwa kwa madini za shaba, bati, lead, chuma na magnesium,licha ya madini hayo, ndani yake kuna dhahabu na fedha ambazo uzito wake ni kilo 18.6 na kilo 38.

Mtaalamu mmoja husika alisema kuwa kengele hiyo ni ajabu duniani katika sekta ya kusubu, utengenezaji wake ni kazi ngumu hata hivi sasa.