中国国际广播电台
Katika miaka ya karibuni wataalamu
walipiga picha ya mji wa Beijing
kutoka angani kwa teknolojia
ya “remote sensing”, waliwaona
dragon wawili waliolala na jitu
mmoja lililo keti kwenye eneo
la mji, hayo yamekuwa maajabu
mawili ya mji wa Beijing.
Picha ya rangi iliyotokana
na teknolojia hiyo inaonesha
kuwa dragon wa kwanza anaundwa
na majengo ya kale ya Beijing
kuanzia jengo la Tiananmen
hadi jengo la Zhonggu. Na
dragon mwingine anaundwa na
mito na mifereji ya Beijing
na kujulikana kwa “dragon
wa maji”.
Ajabu lingine la Beijing
ni taswira ya bustani ya Jingshan
ambayo inaonekana kama jitu
moja lililokaa chini. Bustani
ya Jingshan ilikuwa ya wafalme
na iko katika upande wa kaskazini
mwa majumba ya wafalme wa
zamani. Je hali hiyo ni inatokana
na kusanifiwa au ilitokea
kwa bahati tu? Hilo ni swali
ambalo mpaka sasa halijajibiwa.
|