Sindano ya Mfupa na Mapambao ya Sokwe-Mtu
中国国际广播电台
Katika kipindi cha zama mawe cha zamani kiasi cha miaka elfu 50 iliyopita, binadamu walijua kutengeneza na kutumia sindano. Sindano hiyo ilitengenezwa kwa mfupa. Watafiti waliwahi kugundua sindano ya mfupa huko Ozuina barani Ulaya, lakini sindano ile ilitengenezwa kwa ufundi wa kiwango cha chini sana. Sindano iliyogunduliwa katika pango waliloishi sokwe-mtu ilitengenezwa kwa ufundi mkubwa zaidi.

Sindano hiyo ina urefu wa milimita 82 na unene wa milimita 3, ambayo inafanana na njiti ya kiberiti, sindano hiyo ni laini na yenye ncha kali. Watafiti wanasema kuwa sindano hiyo inatufahamisha kuwa, wahenga walioishi mapangoni walikuwa wanavaa nguo.

Wahenga hao walikuwa wanaishi kwenye mapango milimani miaka zaidi ya elfu 18 iliyopita, walijua kutengeneza na kuvaa vitu vya mapambo. Watafiti waligundua mkufu uliotengenezwa kwa mawe, meno ya wanyama, mfupa wa samaki na simbi za baharini.