中国国际广播电台
Su Shi alizaliwa mwaka 1037
na kufa mwaka 1101, alikuwa
mwenyeji wa Mkoa Sichuan. Baba
yake alikuwa mwanafasihi, kuokana
na kuathiriwa na baba yake,
toka alipokuwa mtoto alikuwa
na ari ya kupigania mustakbali
mzuri wa maisha yake. Baada
ya yeye kushika wadhifa alikuwa
mtetezi wa kufanya mageuzi ili
alitawale taifa kwa amani. Alipokuwa
ofisa wa kisehemu na diwani
wa mfalme alikuwa mwanamageuzi
mwenye juhudi akijaribu kuondoa
sera zenye madhara na kutetea
zile zenye maendeleo.
Kutokana na tabia yake ya
kudhihirisha wazi kila kitu
moyoni mwake na kuthubutu
kusema kinaganaga mbele ya
mfalme, mwishowe alikuwa msingiziwa
katika mivutano kati ya vikundi
vya madiwani wa mfalme. Mara
kadhaa alipewa adhabu ya kufukuziwa
mbali, na kila mara mazingira
ya kuishi yalikuwa mabaya
zaidi. Kutokana na ugumu wa
maisha alikuwa amepata falsafa
ya Confucius, ya dini ya Buddha
na ya dini ya Dao akawa mtu
mwenye moyo mpana wa kujiliwaza
kutokana na maisha yake magumu
na huku alikuwa mtu mwenye
matumaini mema ya binadamu
na kuyapigania katika maisha
yake.
Hulka ya Su Shi ya unyoofu
bila kuficha lolote moyoni
ilisifiwa sana katika kipindi
cha mwisho cha jamii ya umwinyi
nchini China na iliathiri
wasomi kwa miaka 800.
|