中国国际广播电台
Tao Yuanming pia anaitwa Tao
Qian, alikuwa ni mshairi wa
kueleza mandhari ya maumbile.
Alikuwa mtu wa kuridhika na
maisha yake ya umaskini, mwenye
hulka ya unyoofu, wasomi wa
baadaye walimsifu sana.
Baba wa babu wa Yuan Mingyuan
alikuwa ni mwanzilishi wa
Enzi ya Jin Mashariki, babu
yake na baba yake wote walikuwa
ni maofisa. Tao Yuanming alipokuwa
na umri wa miaka minane baba
yake alifariki, hali ya familia
ikawa duni. Alipokuwa mtoto
alikuwa na tumaini kubwa la
kuwa ofisa na kutoa mchango
katika mambo ya kisiasa.
Lakini Enzi ya Jin Mashariki
kilikuwa ni kipindi cha vurugu,
migogoro kati ya maofisa na
ufisadi vilikithiri katika
kasri la mfalme. Ilikuwa muda
mfupi baada ya Tao Yuanming
kuwa na wadhifa alipokuwa
na umri wa miaka 29, alijiachisha
kazi na kurudi nyumbani kutokana
na kutoweza kuvumilia ufisadi
huo.
Maisha ya Tao Yuanming yalikuwa
mabaya siku hadi siku, na
hata alishindwa kuwalisha
jamaa zake kwa kulima, ilimpasa
ajitafutie wadhifa, na alipokuwa
na umri wa miaka 41 alikuwa
ofisa wa wilaya. Lakini kutokana
na hulka yake ya kuchukia
matajiri na kujinyenyekea,
alikuwa madarakani kwa siku
80 tu alijiachisha kazi. Tokea
hapo alikuwa ameacha kabisa
wadhifa na kuishi kwa kutegemea
kilimo.
Maisha yake ya kilimo yalikuwa
mabaya sana, alipokuwa na
umri wa miaka 44 nyumba yake
iliungua, maisha yalikuwa
magumu zaidi. “Kukaa na njaa
katika siku za joto, na kulala
bila mfarishi katika siku
za baridi” ni beti iliyoeleza
hasa umaskini kwenye maisha
yake. Lakini alikuwa na moyo
mtulivu kuvumilia umaskini
huo. Katika kipindi hicho
aliandika mashairi mengi ya
kueleza mandhari ya vijijini.
Kutokana na kalamu yake, kwa
mara ya kwanza maisha ya wakulima
na mandhari ya vijijini ilikuwa
mada muhimu katika maandishi.
Maisha ya uzeeni ya Tao
Yuanming yalikuwa ya kusikitisha
sana, hata mara nyingne alikuwa
anaomba, hata hivyo alipokuwa
maskini sana alikataa wadhifa
kwa mara nyingine tena. Insha
aliyoandika uzeeni “Matembezi
katika Kijiji cha Taohuayuan”
inajulikana kwa wote. Katika
makala hiyo alieleza mvuvi
mmoja aliyepotea njia aliingia
katika kijiji hicho aligundua
baadhi ya watu wanaoishi katika
kijiji hicho, watu ambao kizazi
kwa kizazi waliishi huko kwa
ajili ya kukwepa vurugu za
vita, walikuwa hawajui dunia
ilivyo nje ya kijiji hicho,
wote walikuwa ni watu wenye
juhudi za kazi na waaminifu,
wakiishi maisha ya utulivu
bila wasiwasi. Maisha ya watu
katika kijiji cha Taohuayuan
yaliwakilisha matumaini mema
ya mshairi Tao Yuanming ya
amani badala ya jamii iliyojaa
vurugu za vita.
Mashairi na makala za Tao
Yuanmin zilizobaki ziko zaidi
ya mia moja tu, lakini nafasi
ya mshairi huyo katika historia
ya fasihi ya Kichina ni muhimu
sana.
|