中国国际广播电台
Katika karne ya saba K.K. kitabu
cha kwanza kabisa cha mkusanyiko
wa mashairi “Mashairi ya Kale”
kiliandikwa. Ndani ya kitabu
hicho yalikusanywa mashairi
ya aina mbalimbali ya masimulizi
ya matukio, mapenzi, vita na
nyimbo za kusifu mambo fulani.
Mashairi hayo hayakuandikwa
na mtu mmoja. Kitabu hicho kilikusanya
mashairi 305 yaliyokuwa katika
miaka mia tano.
Mashairi katika kitabu hicho
hapo awali yalikuwa kwa ajili
ya matumizi ya kuimbwa katika
sherehe, burudani na kuonesha
fikra za kisiasa, na baadaye
yalikuwa masomo ya watu wa
tabaka la matajiri. Kusoma
kitabu hicho kulikuwa dalili
ya elimu ya juu. Masomo hayo
yalisaidia sana lugha katika
maingiliano ya kijamii, watu
walikuwa wakitumia beti fulani
za mashairi kueleza maana
yake bila kusema moja kwa
moja. Confucius aliwahi kusema,
“bila kusoma ‘Mashairi ya
Kale’ mtu hawezi kuongea”,
alisifu sana kitabu hicho.
Kwa muhtasari, “Mashairi
ya Kale” ni mwanzo wa fasihi
kubwa ya China, ni dalili
ya ustawi wa fasihi. Mashairi
yake yalihusika na pande mbalimbali,
na lugha yake ni tegemeo muhimu
katika utafiti wa lugha ya
Kichina katika kipindi cha
karne ya 11 K.K. hadi karne
ya sita K.K.
|