Mwandishi wa tamthilia Li Yu
中国国际广播电台

  Katika historia ya fasihi ya milenia kadhaa, walitokea washairi na waandishi wengi wa tamthilia na riwaya, Bw. Li Yu alikuwa mmojawapo.

Li Yu alizaliwa mwaka 1610 katika Enzi ya Ming. Katika miaka alipokuwa na umri wa miaka 30 ndipo mabadiliko ya enzi za kifalme yalipotokea. Enzi ya Qing ambayo ni enzi ya mwisho ya umwinyi nchini China iliiangamiza Enzi ya Ming, na kusababisha msukosuko wa jamii, msukosuko huo uliendelea kwa miongo kadhaa. Maisha ya Li Yu yalikuwa katika mazingira hayo hadi alipokufa mwaka 1680.

Li Yu alifundishwa na fikra za Confucius toka alipokuwa mtoto akitamani kufuata njia iliyochukuliwa na wasomi wengi wa zamani yaani kupata wadhifa kwa kufanikiwa katika mtihani. Lakini bahati mbaya alikutana na mazingira ya wasiwasi wa jamii, alishiriki kwenye mtihani mara kadhaa lakini mara zote alishindwa. Tokea hapo aliacha kabisa njia hiyo, alianzisha duka ili alijipatie kipato kwa kuwasaidia wengine kuandika makala, na akiwa na muda alitunga tamthilia.

Mafanikio makubwa maishani mwa Li Yu ni tamthilia na nadharia ya utungaji wa tamthilia. Maandishi ya tamthilia yaliyobaki ni kumi ikiwa ni pamoja na “Samaki Wayo” na “Mapenzi ya Phoenix”. Tamthilia zake zote ni za kueleza mapenzi na kusifu matumaini ya wapenzi vijana, na kuponda mila ya ndoa iliyoamuliwa na wazazi. Tamthilia zake zinapendwa sana na watazamaji na hata ziliigwa katika nchi za kusini mashariki za Asia, hadi sasa tamthilia zake zinaendelea kuigizwa.

Li Yu licha ya kuwa mwandishi wa tamthilia, yeye pia ni mwananadharia wa utungaji tamthilia na mwandishi wa riwaya. Riwaya zake za “Tamthilia Isiyo na Sauti” na “Jumba la Ghorofa” zinajulikana sana. Katika riwaya zake alitetea usawa kati ya wanaume na wanawake.