中国国际广播电台
Hii ni riwaya iliyoandikwa na
Luo Guanzhong, riwaya hiyo inayojulikana
kwa wote wa China. Luo Guanzhong
aliishi kati ya mwaka 1330 hadi
1400, kwani maisha ya mwandishi
huyo hayajulikani sana.
Riwaya ya "Madola Matatu
ya Kifalme" iliandikwa
kwa msingi wa historia ilivyokuwa
kati ya mwaka 184 hadi 280
nchini China. Wakati huo madola
matatu ya kifalme yaani Wei,
Shu na Wu yalikuwa katika
hali ya kulingana kwa nguvu.
Lakini kila moja lilikuwa
likitaka kuliangamiza lingine
ili kuitawala China nzima,
kwa hiyo vita vilikuwa haviishi.
Kutokana na msingi wa masimulizi
miongoni mwa raia kuhusu vita
baina ya madola hayo matatu
mwandishi Luo Guanzhong alihariri
na kuandika riwaya hiyo kwa
msaada wa maandishi ya historia,
akieleza mivutano iliyotatanisha
kati ya madola matatu katika
mambo ya kijeshi, siasa na
kidiplomasia. Riwaya hiyo
ambayo hasa inaeleza mapambano
ya kijeshi, inavutia kwa hila
za kivita. Kwa ufanisi riwaya
hiyo imesawiri sura za watu
zaidi ya 400.
Riwaya "Madola Matatu
ya Kifalme" sio tu ina
thamani kubwa katika fasihi,
na pia ni maandishi yaliyoeleza
jamii kutoka pande mbalimbali.
Kwa hiyo wasomi wengi zaidi
na zaidi wanachunguza riwaya
hiyo kwa ajili ya kutafiti
historia, fasihi, saikolojia,
hila za kivita, kwa ajili
ya matumizi ya leo. Riwaya
hiyo imetafsiriwa kwa lugha
nyingi na inapendwa sana na
wasomaji.
|