中国国际广播电台
Katikati ya karne ya 18, kilikuwa
ni kipindi cha ustawi mkubwa
katika Enzi ya Qing, lakini
katika kipindi hicho ilitokea
riwaya ndefu iliyoashiria mporomoko
utakaotokea katika jamii ya
kimwinyi, riwaya hiyo ni “Ndoto
katika Jumba Jekundu”.
"Ndoto katika Jumba
Jekundu" ni riwaya iliyoandikwa
na Cao Xueqin ambaye aliishi
kati ya mwaka 1715 hadi 1763.
Hapo mwanzo riwaya hiyo ilienea
katika jamii kwa kunukuu kutoka
wasomaji hadi wengine, kwa
sababu riwaya hiyo ilishukiwa
kuwa ililenga utawala wa wakati
huo, kitabu chake cha kuchapwa
rasmi lilikuwa ni jambo la
baadaye. Mwandishi wa riwaya
hiyo alizaliwa katika ukoo
wa maofisa uliokuwa ukiporomoka
kizazi hadi kizazi. Babu na
baba wa mwandishi huyo wote
walikuwa ni maofisa wakubwa
katika utawala wa kifalme
na walikuwa na uhusiano wa
karibu na ukoo wa kifalme,
lakini hadi miaka wakati ukoo
wa mwandishi huyo ulipoporomoka
kwa madaraka na hadhi, hata
maisha yalikuwa magumu. Wengi
wanaona kuwa Cao Xueqin aliandika
riwaya hiyo kwa mujibu wa
hali ya ukoo wake ilivyokuwa,
na kutokana na umaskini mwandishi
Cao Xueqin alifariki kabla
kumaliza riwayake. Kitabu
hicho kilipoenea kutokana
na kunukuu alikuwapo mwandishi
aliyeitwa Gao E, huyo ndiye
aliyemmalizia riwaya yake
na kuifanya riwaya hiyo kuwa
na sura 120 za sasa.
Riwaya hiyo imeeleza jinsi
jamii ya wakati ule ilivyokuwa
kupitia maelezo kuhusu koo
nne kubwa za "Jia, Shi,
Wang na Xue", hasa maelezo
kuhusu jinsi ukoo wa Jia ulivyostawi
na kuporomoka. Uhodari mkubwa
katika riwaya hiyo ni kueleza
maisha halisi yalivyokuwa
na sura halisi za wahusika
walivyo. Ndani ya riwaya hiyo
wahusika wafikia zaidi ya
400 na kila mmoja ana tabia
na hulka yake mwenyewe, hakuna
aliyefanana na mwingine, ikionesha
ustadi mkubwa wa fasihi wa
mwandishi. Maelezo kuhusu
maisha ya kila siku yanachukuliwa
kama ni maelezo halisi ya
maisha ya wakazi wa Beijing
yalivyokuwa katika karne ya
18. Riwaya ya "Ndoto
katika Jumba Jekundu"
inakubalika kwa wote kuwa
ni kilele cha utunzi katika
fasihi ya kikale ya China.
|