中国国际广播电台
"Jiangger" ni utenzi
wa kabila la Wamongolia na ulitokea
katika karne ya 15 hadi 17.
Mhusika mkuu katika utenzi huo
Jiangger, alipokuwa na miaka
miwili wavamizi wakatili wa
Mangusi waliishambulia sehemu
ya maskani yao, wazazi wake
waliuawa, Jiangger akawa yatima.
Ili kulipiza kisasi kwa ajili
ya wazazi wake, alipokuwa na
umri wa miaka mitatu alianza
kupigana vita huku na huko na
alipokuwa na umri wa miaka saba
alipata ushindi mkubwa, alichaguliwa
kuwa kiongozi wa kabila lao.
Lakini wavamizi wa Mangusi walikuwa
hawakubali kushindwa, walikuwa
mara kwa mara wakifanya uvamizi
dhidi ya kabila la Jiangger.
Jiangger aliwaongoza majemadari
35 na askari hodari elfu 8 na
kuwashinda wavamizi. Jiangger
kwa hekima yake alijenga nchi
iliyotamanika. Kwamba watu wanaoishi
katika nchi hiyo hawazeeki,
mimea inastawi mwaka mzima.
Wananchi wanaishi kwa furaha
tele na kicheko cha furaha kinasikika
kila mahali.
Utenzi huo ulimwelezea shujaa
aliyependwa sana na watu wa
kabila lake kwa akili zake
na ushupavu wake. Huu ni utenzi
wenye taathira kubwa kwa fasihi
ya kabila la Wamongolia, hivi
sasa ni utamaduni unaohifadhiwa
na serikali ya China.
|