中国国际广播电台
Utenzi "Manasi" ulitokea
kati ya karne ya 9 hadi 10 mkoani
Xinjiang. Manasi ni shujaa katika
masimulizi ya mapokeo mkoani
Xinjiang, ni hadithi inayoeleza
Manasi alivyoongoza watu kupambana
na watawala wa kabila jingine
waliowanyanyasa na kupigania
uhuru wa kabila lake. Utenzi
huo una beti laki 2.1 na maneno
milioni 20. Katika utenzi huo
watu zaidi ya 100 walieleziwa
ambao wako wazee waliomwunga
mkono na marafiki, pia wako
watu wabaya, mfalme, wahaini
na mashetani.
Utenzi "Manasi"
umetafsiriwa kwa Kichina kutoka
lugha ya kikabila na baadhi
ya sehemu za utanzi huo zilitafsiriwa
kwa lugha za Kiingereza, Kifaransa
na Kijapan. Kutokana na umaarufu
wa utenzi huo UNESCO iliwahi
kuamua mwaka 1995 kuwa ni
"Mwaka wa Manasi Duniani".
|