Hadithi ya Nuwa Aumba Binadamu

中国国际广播电台

Katika hekaya za kale, kuna hekaya ya jinsi Nuwa alivyoumba binadamu. Nuwa alikuwa ni mungu wa kike mwenye mwili wa binadamu na kichwa cha dragoni.

Inasemekana kuwa baada ya Pangu kutenganisha mbingu na ardhi, Nuwa alitembelea duniani huku na huko, wakati huo duniani kulikuwa na majani, ndege, wanyama na samaki, lakini ilikuwa kimya kabisa kwa sababu kulikuwa hakuna binadamu. Siku moja alipotembea alihisi upweke, aliona ni afadhali aongeze viumbe vyenye sauti na uchangamfu.

Alipoona majani, maua, ndege na samaki, lakini aliona haitoshi, lazima avumbe viumbe vyenye akili nyingi zaidi.

Alipofika kando na mto wa Huanghe, mbele ya maji alijionea sura yake, alifurahi. Aliamua kutumia udongo kufinyanga sura kama yake na aliongeza miguu miwili, kisha alipuliza pumzi sanamu aliyofinyanga, basi sanamu hiyo ikawa na uhai, Nuwa aliita sanamu hiyo kuwa ni binadamu, na ili kutofautisha wanaume na wanawake alipuliza tena. Basi wanawake na wanaume walimzunguka kumshangilia kwa furaha.

Nuwa alitaka kuumba binadamu wengi, basi alifikiri njia moja ya kuwa alitia kamba ndani ya matope kisha akarusha kamba hiyo na kusambaza matope kila mahali, na kina tone la matope likawa mtu mdogo, kwa njia hiyo aliumba watu wengi.

Ingawa duniani kulikuwa na binadamu lakini binadamu waliwezaje kuishi? Na binadamu ana miaka ya kuishi, watawezaje kuendelea? Basi aliwaunganisha wanaume na wanawake kuwa mume na mke. Kwa njia hiyo binadamu wanaendelea kuwepo duniani kizazi kwa kizazi na idadi ya watu inaongezeka.