Houyi Atungua Majua

中国国际广播电台


      Katika zama za kale, mbinguni kulikuwa na majua kumi. Mwangaza mkali ulikausha mimea yote, na watu walikuwa na shida ya kupumua na hata kuzirai. Kutokana na joto kali wanyama wakali walitoka kutoka kwenye mito na maziwa yaliyokauka, na misitu.

Msiba wa binadamu ulimfanya mungu kuwahurumia binadamu, alimwamuru mpiga mishale hodari Houyi kuwaokoa binadamu. Houyi alipewa na mungu upinde mwekundu na mishale myeupe, alishuka duniani akiwa pamoja na mkewe Chang E.

Houyi alishawishi majua kumi yajitokeze moja moja kwa zamu, lakini majua yalikuwa hayasikii. Houyi alikasirika, alianza kupiga mishale, muda si mrefu alitungua majua tisa na kuliacha moja mbinguni. Hivyo binadamu walianza kuishi kwa usalama.

Mchango wa Houyi uliwafanya miungu mingine waone wivu, wakaenda kwa mungu mkuu kumsemea vibaya, mungu huyo alitengana na Houyi na kuamua kuwatenganisha yeye na mkewe na kuwabakiza duniani daima. Houyi aliyeonewa aliishi na mkewe duniani na kuishi kwa kuwinda.

Jinsi muda ulivyopita, Houyi alizidi kusikia vibaya kumkosea mkewe aliyeshushwa duniani kwa sababu yake mwenyewe. Baadaye alisikia kwamba huko kwenye mlima wa Kunlun kuna dawa ya miti shamba ya ajabu, mtu akila dawa hiyo ataruka mbinguni. Houyi alisafiri mbali hadi kwenye mlima huo na mwishowe alipata dawa hiyo. Jambo linalosikitisha ni kwamba dawa hiyo inaweza tu kutumiwa na mtu moja. Houyi alikuwa hataki kuachana na mkewe, alificha dawa hiyo.

Chang E alishindwa kuvumilia maisha magumu duniani. Siku moja alichukua fursa ambayo Houyi alikuwa hayupo nyumbani, alikula dawa hiyo. Mara aliona mwili wake ukaanza kuwa mwepesi na kisha akapaa mbinguni hadi mwezini. Houyi aligundua mke wake alirudi mbinguni alihuzunika sana lakini hakutaka kumpigia mshale, hivyo alikubali kuishi peke yake duniani.

Houyi aliendelea kuishi kwa kuwinda, aliwapokea wanafunzi kadhaa kuwafundisha kupiga mishale. Kati ya wanafunzi, mmoja aliyeitwa Pengmeng alipata maendeleo ya haraka, lakini aliona kuwa daima atakuwa hodari wa pili kama Houyi akikuwepo. Siku moja mwanafunzi huyo alitumia fursa ya Houyi kulewa alimwua Houyi kwa mshale.

Baada ya kufika mwezini Chang E aliishi peke yake pamoja na sungura mmoja mweupe na mti mmoja mkubwa, kila siku alikuwa anakumbuka maisha akiwa pamoja na mume wake duniani, lakini hakuwa na njia ila kukaa upweke mwezini.