Bian He Amzawadia Mfalme Jade
中国国际广播电台


    Mtu aliyeitwa Bian He wa Dola la Chu siku moja alipata kipande cha jade moja kwenye mlima, alikwenda kumzawadia mfalme wake Chuli. Mfalme huyo alimwita fundi wa kuchonga jade athibitishe kama ni jadi ya kweli. Fundi alisema, “Hii sio jade bali ni jiwe la kawaida!” Mfalme aliona Bian He alimdanganya, akamkata mguu wake wa kushoto.

Mfalme Chuli alikufa, aliyerithi kiti cha ufalme alikuwa Wu. Bian He alichukua kipande hicho kwenda kwa mfalme huyo Wu kama ni zawadi. Mfalme Wu alimwita fundi wa jade kuhakikisha kama ni jade ya kweli. Fundi alimwambia mfalme yale yale kwamba ni jiwe la kawaida. Mfalme Wu alikasirika na alimkata Bian He mguu wake wa kulia.

Baada ya mfalme Wu kufariki, Wenwang alirithi kiti cha ufalme. Bian He alichukua jade mikononi alilia siku tatu mfululizo chini ya mlima, machozi yalikauka na hata alitokwa damu. Mfalme Wenwang alisikia habari hiyo alimtuma mtu kwenda kumwuliza, “Watu waliokatwa miguu ni wengi, mbona wewe tu unalia sana?”

Bian He alijibu, “Sililii miguu yangu, bali nalia jade yangu ingesemwa kuwa ni jiwe na kunisengenya kuwa ni mdanganyifu!” Mfalme Wenwang alimwagiza kuchonga jade hiyo, kweli ni jade safi sana. Mfalme Wenwang aliipa jade kwa jina la “Jade ya Bian He”.

Hekaya hii inalenga mwandishi Han Fei mwenye matumaini makubwa ya kisiasa alivyopuuzwa. Lakini pia inamaanisha kuwa fundi wa jade anawajibika kutambua jade ya kweli, watawala wanapaswa kutambua watu hodari, na watoa hazina wawe tayari kunyanyaswa.