Zou Ji Ashindana Uzuri na Mwengine
中国国际广播电台


     Waziri wa Dola Qi aliumbika na sura nzuri. Siku moja asubuhi, alivaa nguo na kuvaa kofia, alijiangalia mbele ya kioo kwa makini, kisha alimwuliza mke wake, “Unaonaje, sura yangu nzuri inaweza kuzidi sura ya Xu kwenye sehemu ya kaskazini ya mji?”

Mke wake alijibu, “Hata zaidi!”

Bwana Xu ni maarufu kwa sura yake ya kuvutia. Zou Ji hakuamini sura yake inavitia zaidi kuliko Bwana Xu, kwa hiyo alimwuliza zaidi mke wake wa pili, “Unaonaje, sura yangu nzuri inaweza kuzidi sura ya Xu?” Mke wake wa pili alisema, “Anawezaje kukuzidi kwa sura?”

Baada ya siku moja, mgeni mmoja alikuja nyumbani, Zou Ji alimwuliza mgeni huyo, “Sura yangu ya ya Bwana Xu ipi nzuri zaidi?” Mgeni alijibu, “Unamshinda!”

Hatimaye, Bwana Xu alikuja nyumbani kwa Zou Ji. Zou Ji alimchunguza Bwana Xu toka utosini hadi miguuni, aliona kuwa yeye mwenyewe hawezi kabisa kushindana na sura ya Xu.

Usiku, Zou Ji alifikiri sana na mwishowe akafahamu, alisema, “Mke wangu alisema sura yangu nzuri, kwa sababu yeye ananipenda; Mke wangu wa pili alisema sura yangu nzuri kwa sababu kuniogopa; Mgeni alisema sura yangu nzuri kwa sababu aliomba nimsaidie kwa shida. Ukweli ni kwamba sura yangu haivutii kuliko sura ya Xu!”

Hekaya hii inamaanisha kuwa mtu anafaa anajifahamu hali yake mwenyewe, asiwaamini watu wa karibu maneno ya kilemba cha ukoka.