Hadithi ya Chura Aliye ndani ya Kisima
中国国际广播电台


   Ndani ya kisima aliishi chura mmoja, kila siku alikuwa na furaha sana. Siku moja alimwambia kasa wa baharini, “Furaha yangu ilioje! Nikitaka kucheza cheza na kuruka ruka ninaweza, matope ndani ya kisima yanafunika tu miguu yangu, na mimi peke yangu nakaa kisima kizima, karibu nyumbani kwangu!”

Kabla kasa hajaingia kisimani mguu mmoja ulikwamwa, akarudisha mguu wake, alisema, “Maili elfu moja pengine unaona mbali sana, lakini bahari ni kubwa zaidi. Katika enzi mbalimbali za kale ukame ulikuwa hutokea lakini bahari haikukauka wala maji hayakupungua, kuishi ndani ya bahari ni furaha sana!”

Baada ya kusikia hayo chura alikodoa macho, aliona yeye ni mdogo sana.

Hekaya hii inalenga watu wasijivunie elimu yao ndogo, na asiwe na furaha tele kwa kupata faida kidogo tu.