Mzee Juha Ahamisha Milima
中国国际广播电台


     Hadithi ya Mzee Juha Ahamisha milima sio ya kweli, lakini inajulikana kwa kila Mchina. Hadithi hiyo iliandikwa katika kitabu kilichoandikwa na mwanafalsafa Lie Yukou wa karne ya tano.

Hadithi yenyewe inasema hivi: Mzee mmoja aliyeitwa Mzee Juha, alikuwa karibu na umri wa miaka 90. mbele ya nyumbani kwake ilikingama milima miwili, mlima mmoja unaitwa Taihang, mwingine unaitwa Wanwu. Watu wa familia yake walipaswa kuzunguka milima hiyo kwenda mahali pengine.

Siku moja, Mzee Juha aliwaita jamaa zake akisema, “Milima miwili mbele yetu inaziba njia yetu, ni bora sote tufanye juhudi kuihamisha, mnaonaje?”

Watoto na wajukuu wake waliposikia aliyosema wakajibu, “Ni sawa uliyosema, tuanze kesho!” Lakini mke wa Mzee Juha alipinga, “Tumeishi na milima hiyo miaka mingi, kwa nini tusiweze kuendelea nayo? Na milima miwili hata inaweza kuhamishwa, mawe tutayaweka wapi?”

Maneno ya mke wa Mzee Juha yaliwafanya wafikiri sana, kweli hilo ni tatizo kubwa. Mwishowe waliamua kupeleka mawe na udongo kwenye bahari.

Siku ya pili, watu wa ukoo wa Mzee Juha walianza kuhamisha milima. Jirani alikuwepo mjane mmoja, alikuwa na mtoto mmoja wa kiume ambaye alikuwa na umri wa miaka saba tu, aliposikia kuhamisha milima alikuja kuwasaidia. Lakini vyombo vya kuhamisha milima vilikuwa vikapu na majembe tu, na bahari iko mbali na nyumbani kwake. Baada ya mwezi mmoja kupita milima haikuonekana kupungua.

Alikuwepo mzee mmoja aliyeitwa Mzee Mwerevu, alipoona Mzee Juha akihamisha milima, alicheka, alisema, “Wewe umekuwa na umri wa miaka mingi, unawezaje kuhamisha milima hiyo?”

Mzee Juha alijibu, “Wewe Mrerevu akili yako si zaidi ya watoto. Ingawa mimi nakaribia kifo, lakini nina watoto, na watoto watazaa watoto, vivyo hivyo haina mwisho, lakini urefu wa milima hauongezeki, jiwe moja likiondolewa milima inakosa jiwe hilo na haliongezeki, tunahamisha siku nenda siku rudi, mwezi mmoja mwezi rudi, mwaka mmoja mwaka rudi, kwa nini tusiweze kuimalima milima hiyo?” Kusikia hayo Mzee Mwerevu alikuwa hana la kusema.

Watu wa ukoo wa Mzee Juha walichimba milima bila kusita kila siku. Kitendo chao kilimhurumisha mungu ambaye alituma miungu miwili wake kushuka na kuibeba milima hiyo kwenye mahali pengine. Hadithi hiyo inasimuliwa hadi leo ikiwaambia watu kuwa wakiwa na nia wanaweza kufanikisha jimbo lolote.