Kuendea Mwelekeo kinyume na Unaotakiwa
中国国际广播电台


    Katika karne ya tano hadi tano K.K. Kipindi cha Madola ya Kivita, nchini China kulikuwa na madola mengi madogo ambayo yalikuwa yalipambana miaka hadi miaka, katika kipindi hiki walitokea wanasiasa wengi ambao walijitahidi kushawishi wafalme waweze kusikiliza na kufuata maoni yao ili kuyashinda madola mengine. Hadithi ya “Kuendea Mwelekeo kinyume na Unaotakiwa” ilitokea katika kipindi hicho katika Dola la Wei ikieleza jinsi waziri Ji Liang alivyomshawishi mfalme wake.

Katika kipindi hiki kila dola lilijitahidi kuwa na nguvu kubwa kuliko madola mengine ili kuyashinda, hali kadhalika Dola la Wei. Mfalme Wei alitaka kushambulia mji mkuu wa Dola la Zhao, Handan. Wakati huo waziri Ji Liang alikuwa akisafiri kikazi katika dola jingine, aliposikia habari hiyo alikuwa na wasiwasi sana. Kwa haraka alirudi nyumbani na bila kuwahi kunawa uso alikwenda kwa mfalme wake.

Mfalme Wei alikuwa akipanga mpango wa vita, alipomwona Ji Liang alikuja kwa haraka, aliona ajabu, alimwuliza, “Una haraka gani hata hukuwahi kuvaa vizuri?” Ji Liang alisema, “Mheshimiwa mfalme, nilipokuja njiani nilikuta jambo la ajabu.” Mfalme Wei aliona ajabu, alimharakisha amweleze jambo lenyewe. Ji Liang alisema, “Sasa hivi niliona mkokoteni uliovutwa na farasi kuelekea kaskazini, nilimwuliza mwendeshaji, ‘unaelekea wapi?' Yule aliniambia ‘Dola la Chu!' Niliona ajabu nikasema, ‘Dola la Chu liko upande wa kusini, mbona unaelekea kaskazini?' Lakini yeye hakujali niliyomwambia, akisema, ‘Farasi wangu ni hodari sana, mwishowe atafika tu Dola la Chu!' Kusikia hayo niliona ajabu zaidi, nilisema, ‘Hata farasi wako ni hodari namna gani, lakini mwelekeo ni kosa.' Alisema, ‘Usiwe na wasiwasi, pesa nilizo nazo zinatosha kutumika njiani.' Nilishindwa kuelewa, nilimwambia, ‘Hata pesa zako ni nyingi namna gani, lakini njia yako sio ya kuelekea Dola la Chu!' Mwendeshaji huyo alicheka kwa kelele, akisema, ‘Hata hivyo, ustadi wangu wa kuendesha mkokoteni ni mkubwa!' Hakusikia niliyomwambia, aliendelea kuelekea kaskazini.” Mfalme alicheka na kusema, “Ni mjinga kweli huyo!” Kisha Ji Liang alisema, “Mheshimiwa, wewe si unataka kuwa kiongozi wa madola yote? Basi inakupasa upate imani ya watu wote. Lakini sasa kwa kutegemea ardhi yako nyingi kidogo, nguvu ya jeshi kubwa kidogo unataka kufanya vita kuwateka ili kutukuza heshima yako, kufanya hivyo kunakufanya uwe mbali zaidi na na lengo lako, ni sawa na mwendeshaji mkokoteni anayetaka kwenda Dola la Chu upande wa kusini, lakini anakwenda upande wa kaskazini, kinyume na mwelekeo anaoutaka!”

Wakati huo mfalme Chu alielewa aliyosema, alifikiri muda akaona ni sawa aliyosema, akafuta mpango wake wa kushambulia Dola la Zhao.

Wachina mara kwa mara wanatumia methali hiyo kueleza vitendo vinavyokwenda kinyume na lengo linalotakiwa.