Masimulizi kuhusu Mlima Wutai
中国国际广播电台

Mlima Wutai ni moja kati ya milima minne maarufu kwa dini ya Buddha nchini China na pia ni sehemu ya utalii.

Mlima Wutai uko mkoani Shanxi, mlima huo una vilele vitano vilivyozunguka kwa duara, na sehemu ya kila kilele ni tambarare kama jukwaa.

Inasemekana kuwa hapo awali hali ya hewa ilikuwa mbaya sana kwenye sehemu ya Mlima Wutai, katika majira ya baridi ilikukwa baridi mzizimo, katika majira ya Spring upepo wenye mchanga unavuma kwa nguvu, katika majira ya joto jua ni kali sana, wakulima walikuwa hawapati chochote cha mazao. Mungu Wen Zhu alikuwa akieneza dini yake huko, alipoona jinsi watu walivyoteseka na hali mbaya ya hewa, aliamua kuibadilisha.

Wen Zhu alisikia kwamba kwenye bahari ya mashariki kulikuwa na jiwe moja ambalo linaweza kubadilisha hali ya hewa, alijigeuza kama sufii akaenda huko kutaka kuazima jiwe hilo.

Wen Zhu alifika bahari ya mashariki, nje ya kasri la mfalme wa dragoni aliona jiwe hilo, aliingia ndani ya kasri na kumweleza ombi lake la kuazima jiwe. Mfalme wa dragoni alimwambia, “Chochote unachotaka kuazima nakubali, isipokuwa jiwe hilo, kwa sababu jiwe hilo lilikuwa chini ya bahari kwa karne kadhaa na ilipatikana kwa miaka mingi. Watoto wangu baada ya kazi wanajiburudisha na badiri kwa jiwe hilo. Ukiondoka na jiwe hilo watoto wangu watasumbua.” Wen Zhu alimshawishi kwa maneno mazuri na kumweleza jinsi watu walivyoteseka kwa hali mbaya ya hewa.

Mfalme aliona vibaya kumkatalia, na huku akifikiri mzee huyo Wen Zhu atashindwa kubeba jiwe hilo zito, basi akamwambia, “Jiwe hilo ni zito sana, sina watu wa kukusaidia, kama ukiweza basi chukua!”

Wen Zhu alimshukuru, alifika mbele ya jiwe na kunong'onona maneno fulani mdomoni, mara jiwe hilo likawa dogo kama gololi, akatia mfukoni na kuondoka nalo. Mfalme wa dragoni alipigwa bumbuazi, akajuta sana.

Alipofika kwenye Mlima Wutai jua lilikuwa kali sana, kutokana na ukame, ardhi ilipasuka. Wen Zhu aliliweka jiwe hilo kwenye bonde, ajabu ilitokea: sehemu zote za kileleni zikawa malisho, hali ya hewa ikawa baridi. Watu walijenga hekalu kubwa. Hadi sasa Mlima Wutai pia unaitwa Mlima wa Baridi.

Mlima Wutai ni hifadhi ya kimaumbile ya kitaifa. Hivi sasa kuna mehekalu 42, kati ya mahekalu hayo, mahekalu ya Nantansi na Foguangsi yamekuwepo kwa miaka 1200.

Mlima Wutai ni sehemu maarufu ya utalii, kuna majabali yenye sura za ajabu, kuna michirizi na miti ya aina kwa aina, kwenye kilele theluji haiyeyuki, hata katika majira ya joto huko hali ya hewa huko ni baridi baridi.