Hekalu Linalokuwa Hewani Mkoani Shanxi
中国国际广播电台


    Kama tujuavyo, mahekalu hujengwa juu ya ardhi, lakini kuna hekalu moja lilijengwa hewani mkoani Shanxi. Hekalu hilo liko karibu na mji wa Tatong mkoani Shanxi, hekalu hilo lilijengwa miaka 1400 iliyopita.

 Hekalu hilo lilijengwa kwenye genge la mlima, linaonekana kama liko hewani ambalo liko mita 50 juu ya ardhi, chini ya hekalu hilo kuna nguzo zaidi ya kumi zinazohimili. Hekalu hilo lina vyumba 40, watu wanapokuwa kwenye hekalu hilo wanahofia kuwa huenda hekalu hilo litaanguka, ingawa sakafu ya mbao inalialia inapokanyagwa lakini hekalu hilo ni madhubuti kabisa.

Juu ya hekalu hilo kilele cha mlima kinajitokeza nje kama mwavuli ukikinga mvua, mafuriko yakitokea katika bonde la mlima hayaathiri hekalu. Ingawa hekalu hilo lilijengwa kwa mbao, lakini lilipita milenia moja salama.

Kwa kweli hekalu hilo halisimamishwi na nguzo zaidi ya kumi, bali linasimamishwa na magogo yaliyogongomelewa ndani ya majabali, na magogo hayo yaliwahi kuloweshwa ndani ya mafuta.

Hekalu hilo lilijengwa kwa kufuata mazingira pembeni. Nyuma ya ukumbi lilichimbwa pango ili kuongeza ukubwa wa ukumbi. Kuna njia nyembamba inayopindapinda mlimani na kufikia hekalu hilo.

Watu watauliza, kwa nini hekalu linajengwa gengeni? Hapo awali sehemu ya hekalu hilo ilikuwa ni kipito, ili kurahisisha waumini wafanye ibada hekalu lilijengwa huko. Zaidi ya hayo, chini ya mlima kuna korongo, na mara kwa mara kuna mafuriko, watu wa kale waliamini kuwa kama hekalu likijengwa huko linaweza kutuliza mafuriko.

Kwenye jabali karibu na hekalu yamechongwa maneno “Ufundi mkubwa wa Gongshu”. Gongshu alikuwa ni fundi mkubwa aliyeishi miaka elfu mbili iliyopita, maneno hayo yanamaanisha kuwa ufundi wa hekalu hilo ni kama ufundi wa Gungshu.