Hadithi kuhusu Magenge Matatu ya Mto Changjiang
中国国际广播电台


      Mto wa Changjiang ni mto wa kwanza mkubwa nchini China na ni wa tatu kwa ukubwa barani Asia. Katika sehemu ya mwanzo na ya kati kuna magenge matatu ambayo kwa jumla yana urefu wa kilomita karibu mia mbili. Mandhari ya kando mbili za magenge hayo matatu inavutia na ni sehemu maarufu ya utalii duniani.

Katika magenge hayo matatu kuna mji mmoja inaoitwa Baidi. Jina hilo lilitokana na hadithi moja, mhusika mkuu katika hadithi hiyo aliitwa Gong Sunshu.

Mwaka 25 China ilikuwa katika hali ya kubadilisha enzi, Enzi ya Han Magharibi ilipinduliwa na uasi wa wakulima na enzi mpya ilikuwa haijaanzishwa, jemadari wa jeshi lililokalia sehemu ya kusini magharibi ya China alisubiri fursa yake ya kunyakua utawala wa China nzima.

Siku moja Gong Sunshu aliota ndoto, kwenye ndoto alisikia mtu mmoja akimwambia, “Utakuwa mfalme wa miaka 12.” Baada ya kuzinduka alipotembea katika bustani yake aliona kuna moshi mweupe unaotoka kisimani, moshi huo ulionekana kama dragoni, Sun Gongshu aliona hii ni dalili ya yeye kupata ufalme, basi alijitawaza kuwa mfalme kwa jina la Baidi, na kuita mji aliokaa kuwa “mji wa Baidi”, na kupanga askari wengi kuulinda.

Gong Sunshu alikuwa na rafiki mmoja mkubwa, aliitwa Ma Yuan. Huyo Ma Yuan alikuwa na elimu kubwa, aliposikia Gong Sunshu amejitawaza kuwa mfalme alikuja kutoka mbali kutaka kuonana naye. Lakini hakutegemea kwamba Gong Sunshu alijigamba na kumwamuru abadilishe nguo yake kwa nguo ya kiraia kabisa, kisha alikutana naye huku akiwa anashangiliwa na askari wake wengi. Gong Sunshu alimteua Ma Yuan kuwa jemadari. Wafuasi wa Ma Yuan walitumai wangepewa nyadhifa fulani, lakini Gong Sunshu aliwaambia kwamba, “Hivi sasa jamii inavurugika sana, siwezi kuwapokea.” Gong Sunshu hakufahamu kuwa huu ndio wakati wa kupokea watu hodari kushauriana mambo makubwa ya taifa.

Wakati huo Liu Xiu alikuwa ameanzisha mamlaka yake, alimwandikia barua Gong Sunshu kumshawishi ajiunge naye. Lakini Gong Sunshu aliona kuwa yeye ni mfalme, anawezaje kusalimu amri, alikataa, Mwaka 37 Liu Xiu aliongoza jeshi lake kumshambulia, Gong Sunshu aliuawa vitani.

Gong Sunshu alikuwa mfalme kwa miaka 12 na baadaye aliuawa. Toka mwanzo mpaka mwisho Gong Sunshu alitawala sehemu ya kusini magharibi kwa miaka 28. Kutokana na kuwa katika muda huo wa miaka 28 jamii ya sehemu hiyo ilikuwa tulivu, na kilimo kilipata maendeleo. Kwa hiyo baada ya Gong Sunshu kufariki wenyeji walimjengea “hekalu la Baidi” kumkumbuka.

Kwenye magenge matatu kuna sehemu nyingi za utalii na masimulizi ya kale. Kuna vilele 12 vya milima, watu waliviita “vilele vya malaika” na walitunga hadithi nyingi kuhusu vilele hivyo.

Hivi sasa miradi ya hifadhi ya maji inatekelezwa katika sehemu ya magenge matatu, kutokana na miradi hiyo, baadhi ya sehemu za utalii zilitoweka, lakini sehemu nyingine za utalii zilitokea.