Hadithi kuhusu Bustani ya Jinci
中国国际广播电台


     Bustani za kale katika sehemu ya China zinajulikana sana, lakini katika sehemu ya kaskazini ya China pia kuna bustani maarufu, bustani hiyo ndio Bustani ya Jinci katika mji wa Taiyuan mkoani Shanxi.

Bustani ya Jinci iko kiungani mwa mji wa Taiyuan upande wa kusini magharibi. Katika bustani hiyo kuna kumbi, majumba ya ghorofa, vibanda, madaraja na maziwa, mandhari ni kama picha ya kuchorwa.

Mwaka 1064 mwanzilishi wa Enzi ya Zhou, mfalme Zhou Wuwang alifariki dunia miaka miwili baada ya yeye kuangamiza Enzi ya Shang, mtoto wake wa kiume alirithi kiti chake cha ufalme, aliitwa mfalme Zhou Chengwang. Kwa sababu alikuwa mtoto mdogo, kila siku alibebwa na waziri Zhou Gong kupanda jukwaa kuwapokea salaam za mawaziri katika kasri, na mambo ya serikali yaliendeshwa na waziri Zhou Gong. Waziri huyo alikuwa mwaminifu, alituliza mara kadhaa uasi na alitumia makini sana kumlea mtoto huyo ili awe mfalme hodari.

Siku moja, mtoto huyo Zhou Chengwang alitumia jani moja la mti na kumwambia ndugu yake Shu Yu, “natumia jani hilo kukuteua uwe mtemi.” Baada ya siku kadhaa Zhou Gong alisikia habari hiyo, alimwomba Zhou Chengwang achague siku kumteua ndugu yake Shu Yu. Lakini Zhou Chengwanga alisema, “Nilimtania tu.” Kwa makini Zhou Gong alisema, “Mfalme haifai kufanya masihara. Maneno ya mfalme yote yataandikwa na yatatekelezwa kwa lazima.” Tokea hapo Zhou Chengwang alikuwa mtu wa makini sana, na kweli baadaye alimteua mdogo wake Shu Yu kuwa mtemi wa sehemu ya Tangdi.

Sehemu ya Tangdi iko katika mkoa wa Shanxi. Baada ya Shu Yu kuwa mtu mzima aliendesha mambo vizuri, alistawisha kilimo na kuendeleza umwagiliaji, watu wa huko walikuwa na maisha mazuri. Baada ya Shu Yu kufariki, watu walimjengea bustani ili kumkumbuka. Bustani hiyo ndio bustani ya Jinci.

Mwaka wa kujenga bustani hiyo haubainiki, lakini maandishi ya kale yaliyohusu bustani hiyo yalikuwa ya Enzi ya Wei kaskazini (466-572), kwa hiyo bustani hiyo imekuwa na miaka zaidi ya elfu moja. Katika kipindi hicho cha zaidi ya miaka elfu moja, majengo ndani ya bustani hiyo yaliwahi kukarabatiwa mara kadhaa na kuongezwa. Mwaka 646 mfalme wa pili wa Enzi ya Tang Li Shimin aliiandikia bustani hiyo maelezo, na kuongeza majengo.

Ndani ya bustani hiyo kuna majengo yenye enzi tofauti, na pia kuna mti mmoja uliopandwa katika Enzi ya Sui (karne ya 11 K.K. hadi karne ya 8 K.K,), mti huo umekuwa na miaka karibu elfu mbili, mpaka sasa bado ni mzima majani yanastawi, mti huo pamoja na ziwa la maji ya chemchemi yamefanya mandhari ya bustani ijulikane na kuwavutia watalii wengi.