Mao Sui Ajipendekeza kwa Kazi
中国国际广播电台


       Kuna usemi wa Kichina unaosema “kama kweli ni dhahabu, basi itang'ara tu”. Hadithi ya Kichina ya “Mao Sui ajipendekeza kwa kazi” ndio inaeleza usemi huo.

Katika Kipindi cha Madola ya Kivita, mji mkuu wa Dola la Zhao Handan ulivamiwa na askari wa Dola la Qin lenye nguvu, mji ulikuwa katika hali ya kutekwa.

Ili kuuokoa mji wa Handan mfalme wa Dola la Zhao alitaka kushirikiana na Dola la Chu lenye nguvu vile vile kupambana na Dola la Qin. Alimtuma mtoto wake Ping Yuanjun kwenda kumshawishi mfalme wa Dola la Chu.

Kabla ya safari, Ping Yuanjun alitaka kuchagua washauri hodari 20 kati ya mawaziri, lakini mwishowe alichagua mahodari 19 tu. Wakati huo alikuja mtu mmoja bila kualikwa, alijipendekeza kujaza pengo la mtu mmoja. Huyo alikuwa Mao Sui.

Ping Yuanjun alimwangalia na kumwuliza, “Wewe ni nani? Una shida gani nami?”

Mao Sui alimwambaia, “Jina langu ni Mao Sui. Nimesikia utakwenda Dola la Chu kwa ajili kuuokoa mji wa Handan, napenda kufuatana nawe.”

Ping Yuanjun alimwuliza, “Umefanya kazi kangu kwa muda gani?”

Mao Sui alijibu, “miaka mitatu.”

Ping Yuanjun alisema, “Muda wa miaka mitatu si mfupi. Mtu akiwa hodari ni kama sindano ya viatu iliyotiwa mfukoni ambayo itatoboa mfuko mara moja. Lakini wewe umekuwa na miaka mitatu hapa, na sijasikia uhodari wako. Safari yangu ya kwenda Dola la Chu inahusika na msaada wa jeshi na hatima ya taifa, mtu asiye hodari haifai kwenda huko, basi wewe baki basi.”

Ping Yuanjun alisema moja kwa moja. Lakini Mao Sui alimjibu kwa uhakika, “Umekosea, sio mimi sina uhodari, bali wewe hukunitia mfukoni. Ungenitia mfukoni, uhodari wangu ungeonekana kama sindano ya viatu.”

Kutokana na mazungumzo, Ping Yuanjun alimwamini na kukubali. Baada ya kupata washauri 20 alifunga safari nao kwenda kuzungumza na mfalme wa Dola la Chu. Baada ya kuwasili Dola la Chu Ping Yuanjun alimweleza vilivyo haja yake ya kupata ushirikiano wa Dola la Chu ili kupambana na Dola la Qin, lakini mfalme wa Dola la Chu alikuwa kimya. Mazungumzo yao yaliendelea mpaka mchana bila matokeo yoyote. Wafuasi 20 walisubiri nje wakiwa na wasiwasi.

Mao Sui alifuatana na Ping Yuanjun kwa kujipendeza, kwa hiyo wengine 19 walimdharau, wakifikiri kuwa alijitukuza tu. wakati huo walitaka kumwadhiri,

“Ndugu Mao, mazungumzo yamekuwa marefu, unaonane uingie na kuona hali ilivyo?”

Mao Sui alikubali. Alichomeka kitara kiunoni na kufika mbele ya mfalme wa Dola la Chu, alisema,

“Mheshimiwa mfalme, ushirikiano wa Chu na Zhao ni wa lazima. Hilo ni jambo la maneno mawili matatu tu kwa kufanya uamuzi. Lakini toka asubuhi mpaka sasa hujaamua, kwa nini?”

Kujitokeza kwa Mao Sui kulimkasirisha mfalme wa Chu, badala ya kuongea naye, alimwuliza Ping Yuanjun kwa hasira,

“Ni nani huyu?”

Ping Yuanjun alijibu, “Ni mfuasi wangu.”

Kwa hamaki, mfalme Chu alimkaripia Mao Sui,

“Mimi nazungumza bwana wenu, wewe ni kama nani kujiingiza katika mazungumzo yetu!”

maneno ya mfalme Chu yalimhamakisha Mao Sui, alitoa kitara chake kutoka ala, akapiga hatua mbele ya mfalme na kusema kwa ukali,

“Mheshimiwa, sababu yako ya kuthubutu kunipokea si unaona dola lako kubwa? Na kutegemea pembeni mwako wako walinzi? Lakini sasa nakuambia, yote hayo hayasaidii kitu ninapokuwa mbele yako kwa kitara, uhai wako uko mkononi mwangu!”

Mfalme Chu alilowa jasho kwa hofu, alikuwa kimya.

Mao Sui alisema, “Dola la Chu lina nguvu, linastahili kuwa mwamba kati ya madola yote, lakini rohoni mwako unaogopa Dola la Qin. Dola la Qin lilishambulia dola lake mara nyingi na kunyakua ardhi yako, ni aibu namna gani hiyo! Hata sisi watu wa Dola la Chu tunakuonea fedheha. Sasa tumekuja kuomba ushirikiano wako kwa ajili ya kuuokoa mji wa Handan, lakini huku tunakusaidia kulipiza kisasi. Lakini wewe ni mhofu kama hivi, huoni aibu!”

Kutokana na maneno ya Mao Sui, mfalme Chu alisikitika sana.

Mao Sui aliongeza, “Mheshimiwa mfalme, vipi sasa? Utakubali kushirikiana nasi kupambana na Dola la Qin?”

“Nakubali, nakubali!” mfalme akajibu haraka.

Baada ya Dola la Chu na Zhao kutia saini mkataba wa kushirikiana kupambana na Dola la Qin, akina Ping Yuanjun wakarudi mjini Handan na kumwambia mfalme wa Dola la Chu,

“Bahati njema Mao Sui alifuatana nami, kwa ulimi wake ametupigia jeki kuliko nguvu za askari milioni moja.”

Kabla ya siku tatu kupita, jina la Mao Sui lilienea miongoni mwa watu wa mji wa Handan. Baadaye methali hiyo hutumika kueleza kuwa mtu mwenye uwezo anajipendekeza kwa kazi.