Hadithi ya “Msichana Jirani Amchungulia Song Yu”
中国国际广播电台

Katika historia ya China alikuwepo mwandishi mmoja mkubwa wa Dola la Chu, aliitwa Song Yu. Inasemekana kuwa huyo Song Yu alikuwa mwanamume mzuri kwa sura. Mwandishi huyo aliwahi kuandika makala moja ya kuvutia kwa jina la Msichana Jirani Amchugulia Song Yu.

Hadithi inasema hivi: Song Yu na Deng Tuzi wote walikuwa maofisa waliokuwa na uhusiano wa karibu na mfalme Chu. Deng Tuzi alimwonea wivu Song Yu kutokana na uhodari wake na mara kwa mara alimsema vibaya mbele ya mfalme. Alimwambia mfalme, “Song Yu ana sura ya kuvutia, ana elimu kubwa, lakini ni mwasherati. Kwa hiyo wewe mfalme kabisa usimruhusu aende kwenye ua wa nyuma mahali wanapoishi mahawara wako, ama sivyo atafanya matata.”

Mfalme alimwita Song Yu mbele yake, na kumwuliza ili athibitishe kama ni kweli. Song Yu alisema, “Sura yangu nzuri nilizaliwa nayo, elimu yangu nimepata kutokana na kusoma sana, ama kuhusu uasherati sina kabisa.”

Mfalme Chu alimwuliza, “Una ushahidi?”

Song Yu alijibu, “Warembo wanapatikana zaidi katika dola lako la Chu, na warembo hao wengi zaidi wanapatikana katika maskani yangu Chenli, na huko Chenli, mrembu maafuru ndio jirani yangu. Mrembo huyo akiwa urefu kidogo anapita kiasi, akiwa na ufupi kidogo atakuwa mfupi. Akijipodoa anaonekana mweupe kupita kiasi akipaka kidogo rangi nyekundu ataonekana mwekundu kupita kiasi. Meno yake, nywele zake na vitendo vyake, vyote vinavutia sana. Akitabasamu anawalewesha wanaume wote. Lakini mrembo huyo mara nyingi alinichungulia kwa miaka mitatu, na mimi nilikuwa baridi tu. Nawezaje kuwa mwanasherati? Ukweli ni kwamba mwasherati ndio Deng Tuzi.”

Mfalme Chu alitaka kufahamishwa zaidi. Song Yu alisema, “Mke wa Deng Tuzi hana sura nzuri, lakini alimpenda mara moja alipomwona, na walizaa watoto watano.” Baada ya kusikia hayo, mfalme Chu hakujua la kusema.

Song Yu aliandika maandishi mengi, lakini sasa vimebaki vitabu zaidi ya kumi tu. Kitabu chake maarufu ni “Utenzi wa Malaika”.