Chura Anayecheza na Dragoni
中国国际广播电台


      Katika Enzi ya Han Mashariki, matetemeko ya ardhi yalikuwa yanatokeaa mara kwa mara. Kutokana na maandishi ya hostoria, tokea mwaka 89 hadi 140, katika muda wa miaka zaidi ya hamsini yalitokea matetemeko 33, na tetemeko lililotokea mwaka 119 lilikuwa kubwa sana. Mfalme wa enzi hiyo alidhani kuwa pengine watu walimkosea mungu, kwa hiyo alizidi kuwatoza kodi na kufanya ibada. Kulikuwa na mwanasansi mmoja aliyeitwa Zhang Heng, aliona kuwa tetemeko la ardhi ni hali ya kijiografia, kwa hiyo alizidi kufanya utafiti kuhusu tetemeko la ardhi.

Kutokana na utafiti wake, mwaka 132 alivumbua chombo cha kwanza duniani cha kutoa dalili ya matetemeko ya ardhi.

Chombo cha kutoa dalili ya matetemeko ya ardhi kiliundwa kama mtungi, kipenyo chake karibu mita moja, kwenye mtungi huo kuna dragoni wanane wakitazama mielekeo minane, na kila dragoni alikuwa ameng'ata gololi moja ya shaba, na chini ya dragoni kuna chura aliyetanua midomo, kama tetemeko likitokea kwenye mwelekeo fulani basi gololi hiyo inadondokea mdomomi mwa chura.

Mwaka 133, mji wa Shenyang ulikumbwa na tetemeko, chombo hicho kilitoa dalili, na baadaye mji huo ukikumbwa na matetemeko mara tatu na kila mara chombo hicho kilikuwa hakikosi kutoa dalili. Mwezi Februari, mwaka 138, Zhang Heng aligundua gololi iliyokuwa mdomoni mwa dragoni upande wa magharibi ilidondoka, baada ya siku tatu tarishi wa mji wa Luoyang magharibi mwa China alikuja kupiga ripoti kwamba huko kulitokea tetemeko la ardhi. Watu wanaita chombo hicho kuwa ni “Chura Anayecheza na Dragoni”.