Kuazima Mishale kwa Mashua Zenye Sanamu za Mabua
中国国际广播电台


       Katika karne ya kwanza K.K. nchini China kulikuwa madola matatu ya kifalme kwa pamoja, madola hayo yalikuwa ni Wei, Shu na Wu. Dola la Wei liko kwenye sehemu ya kaskazini, Dola la Shu liko katika sehemu ya magharibi, na Dola la Wu liko sehemu ya kusini. Mwaka mmoja, Dola la Wei lilishambulia Dola la Wu, na askari walipokaribia Dola la Wu walipiga kambi karibu na mto ili kusubiri nafasi nzuri kufanya mashambulizi.

Jemadari mkuu wa Dola la Wu aliitwa Zhou Yu, baada ya kufahamu hali ya maadui aliamua kukinga maadui kwa mishale. Mishale ilikuwa ni lazima iwe laki moja, lakini katika muda mfupi inawezaje kutengeneza mishale hiyo?

Wakati huo jemadari Zhu Geliang wa Dola la Shu alikuwa ziarani katika Dola la Wu. Zhu Geliang alikuwa mwenye hekima sana, Zhou Yu aliomba ushauri kutoka kwake. Zhu Geliang alimwambia, siku tatu inatosha. Wote waliona ahadi ya Zhu Geliang ni mzaha. Lakini Zhu Geliang aliahidi kuwa kama akishindwa atakubali kukatwa kichwa. Zhu Geliang alimwagiza waziri Lu Su wa Dola la Wu atengeneze mashua ishirini, na kila mashua wapande askari na kufunga mabua ya majani kama sanamu.

Zhu Geliang alikuwa hana shughuli mpaka siku ya tatu. Katika siku ya tatu usiku alimwambia Lu Su, “Twende kuchukua mishale.” Lu Su aliuliza, “Wapi?” Zhu Geliang alitabasamu na kusema, “Utajua mwenyewe.” Katika usiku huo ukungu ulikuwa mnene, giza totoro, Zhu Geliang aliamuru kuendesha mashua haraka, mashua hizo zilipangwa kwa mstari mmoja, kisha aliwaamuru askari wapige kilele na kupiga ngoma. Lu Su aliogopa sana alisema, “Mashua zetu ni ishirini tu na askari wachache, jeshi la Wei likitushambulia tutashindwa vibaya.” Zhu Geliang alimwambia, “Usiwe na wasiwasi, jeshi la Wei halithubutu kutushambulia katika ukungu mene na giza namna hii.”

Askari waliposikia kelele na ngoma, jemadari Cao Cao aliamua kuzuia mashambulizi kwa mishale, askari kiasi cha elfu kumi walipiga mishale kwenye ukingo wa mto, mishale ilikuwa mingi kama mvua na kuchomeka kwenye sanamu za mabua. Kwa kuona idadi ya mishale imetosha, Zhu Geliang aliamuru kurudi kabla ya ukungu kutoweka.

Kabla msafara wa mashua kufika kwenye ukingo wa mto, jemadari Zhou Yu alikuwa amekwisha panga askari kusubiri kuchukua mishale.