“Mbinu ya Mji Mtupu”
中国国际广播电台


      Nchini China Zhu Geliang anajulikana kwa watu wote wa China, fulani akifananishwa na Zhu Geliang anasifiwa kwa akili zake.

Katika karne ya pili K.K. nchini China kulikuwa na madola matatu kwa pamoja, nayo ni Wei, Shu na Wu. Kipindi hiki kinaitwa “Kipindi cha Madola Matatu ya Kifalme”. Madola hayo yalipigana mara kwa mara, lakini hakuna hata moja lililoweza kuliangamiza lingine. Zhu Geliang alikuwa ni jemadari mkuu wa Dola la Shu, alijulikana kwa mbinu zake za kivita.

Mfalme wa Dola la Wei alipofahamu kuwa mji wa Dongcheng wa Dola la Shu ulikuwa na upungufu wa askari ambao hawakufikia hata elfu 10, alimwagiza jemadari Sima Yi kuongoza askari zaidi la laki moja kuushambulia mji huo. Mfalme wa Dola Shu alipopata habari hiyo alishikwa na wasiwasi, kwani askari elfu 10 kupambana na askari laki moja hawafui dafu, lakini kuhamisha askari kutoka mahali mengine wakati hautoshi. Wakati huo alitumaini Zhu Geliang angepata njia ya kuuokoa mji wake.

Zhu Geliang alichemsha sana ubongo, kisha aliamuru wenyeji wote waondoke mjini na kwenda kwenye mahali fulani, kisha alifungua mlango wa mji wazi na kusubiri maadui. Muda ulikuwa si mrefu askari walioongozwa na Sima Yi walifika kwenye mji wa Xicheng. Hapo kabla Sima Yi alifikiri hakika atawakuta askari wengi lakini aliona mlango wa mji wa Xicheng wazi kabisa, na ndani ya mji kulikuwa hakuna mtu hata mmoja. Alibabaika, alifikiri kuwa Zhu Geliang ni mtu mjanja, asidanganywe naye. Baada ya dakika chache aliona Zhu Geliang alitokea juu ya ukuta wa mji, alikaa na kukanza kucheza kinanda chake. Wakati huo Sima Yi alibabaika zaidi.

Sima Yi alipoona jinsi Zhu Geliang alivyokuwa mtulivu, alidhani hakika ndani ya mji walificha askari wengi, wakati huo alisikia sauti ya kinanda iliongezeka na muziki ulikuwa unapigwa haraka zaidi. Sima Yi aliona kuwa muziki huo ndio ishara ya kufanya ushambulizi, kwa haraka aliwaamrisha askari wake warudi. Hivyo Zhu Geliang aliulinda mji wa Xicheng bila kutumia askari hata mmoja. Hii ndiyo hadithi ya “Mbinu ya Mji Mtupu”.

Kuna hadithi kuhusu Zhu Geliang ni nyingi, na nyingi zinatokana na riwaya ya kale “Madola Matatu ya Kifalme”.