Zhou Yafu Aushinda Uasi wa Watemi Saba
中国国际广播电台


  Kuna usemi unaosema: Mbuzi anayeongoza kundi la simba anashindwa kwa simba anayeongoza kundi la mbuzi. Usemi huu unaeleza kuwa jemadari ni muhimu sana katika vita.

Katika karne ya pili K.K. Enzi ya Han Magharibi ilikuwa na uhusiano mzuri na kabila la Xiongnu lililoko katika sehemu ya magharibi. Lakini baadaye kutokana na kuchokozwa na wengine, kabila hilo lilikata uhusiano na Enzi ya Han Magharibi. Mwaka 158 askari wa kabila la Xiongnu walifanya mashambulizi kwenye mpaka. Mfalme Han Wendi wa Enzi ya Han Magharibi alituma majemadari watatu wakiongoza askari kupambana na askari wa kabila la Xiongnu, na ili kulinda mji mkuu Chang An aliagiza majemadari wengine watatu kupiga kambi karibu na mji mkuu.

Siku moja mfalme Han Wendi akifuatana na maofisa alikwenda kuwakagua kambi za majemadari walio karibu na mji mkuu. Alipofika kwenye kambi ya jemadari mmoja aitwaye Liu Li, askari walifanya sherehe kubwa kumkaribisha mfalme bila kuzuiliwa mlangoni. Kisha mfalme alifika kambi ya pili, mfalme na wafuasi wake waliingia moja kwa moja ndani ya kambi bila kuulizwa. Mwishowe mfalme alifika kwenye kambi ya tatu iliyoongozwa na Zhou Yafu, mfalme alizuiliwa na askari waliokuwa tayari kwa kupigana, maofisa wa mfalme waliwakemea, “Huyu ni mfalme!” Lakini askari walijibu, “Tunasikiliza amri ya jemadari wetu tu. Bila ruhusa ya jemadari wetu yeyote haruhusiwi kuingia kambini.” Baadaye Zhou Yaping alitoa amri ya kumruhusu mfalme na wafuasi wake waingie.

Baada ya kuingia kambini, Zhou Yafu hakupiga magoti kama wengine walipomwona mfalme, alisema, “Kutokana na nguo ya kivita, sitapiga magoti.” Mfalme alikubali. Baada ya kuwasalimu askari, mfalme na wafuasi wake waliondoka. Njiani maofisa walisema kwa hasira, “Huyo Jemadari Zhou Yaping ni mjeuri, hata mfalme lazima apate ruhusa yake kuingia kambi yake.” Lakini mfalme alisema, “Huyo ndio jemadari hasa! Tukiwa na majemadari kama yeye maadui hawatathubutu kutushambulia.”

Mwaka wa pili, mfalme Han Wendi alipata ugonjwa mzito, alimwita mtoto wake na kumwambia, “kama kutatokea vurugu, mwachie Zhou Yafu aongoze askari, atashinda tu.” Siku chache baadaye mfalme alifariki. Kutokana na mfalme mpya alikuwa kijana watemi wa makabila saba walitumia fursa hiyo kufanya uasi wakijaribu kunyakua kiti cha ufalme. Lakini Zhou Yaping alikaa kimya, mfalme mpya kwa mara kadhaa alimwamrisha apambanane na watemi hao, lakini Zhou Yaping alitulia tu. Zhou Yaping alimwambia mfalme mpya, kutokana na uasi wao sio wa halali, uasi huo hautakuwa na muda mrefu. Kweli muda mfupi baadaye askari wa uasi walipoona Zhou Yaping alikaa kimya hawakuthubutu kufanya ushambulizi.

Mwishowe, watemi saba waliongoza askari wao kurudi, lakini papo hapo Zhou Yaping aliamrisha jeshi lake kuwafukuza na kuwaua.

Baada ya kutuliza uasi wa watemi saba, Enzi ya Han Magharibi ilipata ustawi mkubwa katika historia ya China.